Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Prof. Riziki Shemdoe amewakabidhi eneo la Ujenzi Vikosi vya Ujenzi kwa ajili ya  kuanza rasmi ujenzi wa jengo la Ofisi ya Rais-TAMISEMI.


Makabidhiano hayo yalifanyika Tarehe 30.10.2021  kwenye Makao Makuu ya Ofisi ya Rais TAMISEMI yaliyopo katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.


Prof. Shemdoe amesema jengo hilo litakua la ghorofa sita na litajengwa kwa muda wa miezi 24.


“Mkandarasi atakayejenga jengo hilo ni Vikosi vya Ujenzi kutoka Wizara ya ya Ujenzi na Uchukuzi huku mhandisi mshauri akiwa ni Wakala wa Majengo Tanzania( TBA) na jengo hilo litagharimu shilingi bilioni 23 ukijumuisha gharama za Mshauri” amesema Shemdoe.


Aliongeza kuwa walioomba kazi hiyo walikuwa ni Vikosi vya Ujenzi, Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) , Suma JKT na Mzinga Cooperation lakini aliyefanikiwa kuipata kazi hiyo ni Vikosi vya Ujenzi.


Mkandarasi ambaye ni Vikosi vya Ujenzi amekabidhiwa eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 29,000 lililo pembeni kidogo mwa jengo la muda la Ofisi ya Rais TAMISEMI na kazi za ujenzi  zitaanza rasmi tarehe 01.01.2021.


Shemdoe amesisitiza ubora wa kazi huku thamani ya fedha ikionekana pamoja na kwenda na muda wa mkataba.

Sambamba na kusaini Mkataba wa Ujenzi Vikosi vya Ujenzi wameshakabidhiwa eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 29,000 lililo pembeni kidogo mwa jengo la muda la Ofisi ya Rais TAMISEMI na mkataba huo unaanza rasmi tarehe 01.01.2021.


Shemdoe amesisitiza ubora wa kazi huku thamani ya fedha ikionekana pamoja na kwenda na muda wa mkataba.

Share To:

Post A Comment: