Saturday, 9 October 2021

MBUNGE NEEMA LUGANGIRA AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUUNGA MKONO HOJA YA MAHAKAMA YA FAMILIA


Rais Samia Suluhu akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki cha Mahakama ya Tanzania Oktoba 6 mwaka huu Rais Samia 
Rais Samia Suluhu akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki cha Mahakama ya Tanzania Oktoba 6 mwaka huu Rais Samia 
Rais Samia Suluhu akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki cha Mahakama ya Tanzania Oktoba 6 mwaka huu Rais Samia  kulia ni Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Juma .

Rais Samia Suluhu akikata akizinduzi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki cha Mahakama ya Tanzania Oktoba 6 mwaka huu Rais Samia  kulia ni Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Juma 


KAULI ya Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Asasi za Kiraia Tanzania (NGOs) Neema Lugangira  kuhusu mikakati ya Serikali kufanyia kazi changamoto kubwa iliyopo ya suala zima la Matunzo kwa Watoto imeonekana kuungwa mkono na Rais Samia Suluhu Hassan na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Juma .


Hatua ya uungwaji mkono huo inatokana na kauli za viongozi hao kwa nyakati tofauti wakati wa Uzinduzi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki cha Mahakama ya Tanzania Oktoba 6 mwaka huu Rais Samia aligusia suala hilo.

 
Mbunge Neeema Lugangira alisema katika hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan alisema Masuala ya Kifamilia ikiwemo mirathi, ndoa, talaka, malezi na matunzo ni jambo kubwa mno kwa sababu wanawake na watoto wamekuwa wakiteseka sana.

 

“Katika hotuba yake Mhe Rais Samia Suluhu Hassan alisisitiza masuala ya kifamilia ikiwemo miradi, ndoa, talaka, malezi na matunzo ni jambo kubwa kwa sababu wanawake na watoto mmekuwa mkiteseka sana” Alisema

 
Kwa kuonyesha umuhimu wa suala hilo Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki alisema kwa nyakati tofauti Chama cha Wanasheria Wanawake - TAWLA, Chama cha Wanahabari Wanawake - TAMWA na Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania wameomba ianzishwe Mahakama Maalum yakushughulikia Mashauri ya Kifamilia.

 

Hata hivyo wakati akiwa Bungeni tarehe 21/5/2021 Mbunge Neema Lugangira aliuliza Serikali kuhusu mikakati yake ya kufanyia kazi changamoto kubwa iliyopo ya suala zima la matunzo kwa watoto na baada ya kupokea Majibu ya Serikali aliikumbusha Serikali juu ya ukubwa wa changamoto na kuishauri ianzishe Mahakama ya Familia 

 

Hata hivyo pia katika Mkutano NGOs (29/9/2021), Mbunge Lugangira alisisitiza umuhimu wa Mahakama ya Familia ili wanawake na watoto kupata haki yao ya kisheria na hili hitaji linaendana kabisa na dhamira ya Mhe Rais Samia Suluhu Hassan ya kuimarisha upatikanaji wa haki ya kisheria kwa wanawake. 

Mbunge Lugangira alimalizia kwa kumshukuru sana Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutambua changamoto kubwa wanazopitia wanawake na kuwa mstari wa mbele katika kuzipatia uvumbuzi wa haraka. 

- MWISHO -

No comments:

Post a Comment