Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Kamoli akizungumza na Wakazi wa Kata ya Kipawa
Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Kamoli akikagua kivuko kinachotumiwa na waenda kwa miguu katika mto Msimbazi eneo la Kipawa
Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Kamoli akitembea mtaa kwa mtaa kujionea miundombinu ya kata ya Kipawa ambayo mradi wa DMDP itaitengeneza
Wakazi wa Kata ya Kipawa wakifuatilia mkutano wa hadhara wa mbunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Kamoli uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi karakata


 Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Ladislaus Kamoli leo Jumapili Oktoba 3, 2021 ameendelea na ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na kufanya mkutano wa hadhara katika kata ya Kipawa.

Ziara ya Bonnah ilianza kwa kutembelea kivuko Cha Zanzibar Cafe na baadae alikagua kivuko cha Bonde la Baraka,ambapo alishuhudia namna vivuko hivyo vilivyo na umuhimu wa kujengwa ili viwe vya kudumu.

Mbunge huyo alimwelekeza Diwani ashirikiane naye ili wachukue hatua za makusudi kuwasiliana na TARURA kwa ajili ya ujenzi wa vivuko hivyo.

Ziara ya Mbunge ilihitimishwa na Mkutano wa Wananchi wa hadhara uliyofanyika Mtaa wa Uwanja wa ndege katika viwanja vya Shule ya Msingi Karakata, ambapo Mhe Mbunge alisema kuwa kata ya Kipawa ni miongoni mwa kata zitakazofaidika na Ujenzi wa kingo za mto Msimbazi ambao ujenzi wake utagharimu zaidi ya $120 Milioni (Dola za kimarekani million mia moja na Ishirini)

Mhe.Bonnah ametumia mkutano huo kuelezea namna fedha alizozitoa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan shilingi milioni mia tano (500,000,000) kwa kila Jimbo ili kujenga miundombinu zitakavyotumika jimboni Segerea.

Amesema katika Jimbo la Segerea, fedha hizo zimeelekezwa kujenga barabara ya Airport Karakata kwa kiwango Cha lami ambayo ilikuwa kilio cha muda mrefu na ikizingatiwa barabara hiyo ni muhimu sana, kwa kuwa ndiyo lango la Tanzania na nchi zingine.

'Ujenzi wa barabara hii utaanza baada ya Mradi wa SGR kukamilika kwakuwa wao wanategemea kujenga Daraja katika eneo hili. Na aliongeza pia kwa mujibu wa TRC Mkandarasi atakamilisha ujenzi wa daraja siku chache zijazo.

Bonnah Amesema kuwa milion 500 zilizotolewa na Mhe Rais Siyo za mwisho kwa kuwa anafahamu namna Mhe. Rais Samia alivyodhamiria kuijenga miundombinu na hasa barabara za mitaa. Na kwa jimbo la Segerea watakuwa wanazitumia fedha hizo kila zitakapopatikana kujenga barabara za Lami ambazo zitakuwa alama na ukumbusho kwa kazi nzuri ya Mhe Rais kwa wananchi kwa kuwa barabara hizo ni za kudumu muda mrefu.

Bonnah aliongeza pia kuwa kuzigawa fedha hizo ili zinunue vifusi yasingekuwa maamuzi sahihi ya matumizi yake maana barabara za vifusi huhitaji kukarabatiwa kila mwaka baada ya mvua.

Amewaomba wanasegerea kuwa wavumilivu kwa kuwa barabara nyingi za mitaa ndani ya Jimbo hilo tayari zimeingizwa katika mradi wa DMDP awamu ya tatu na zitajengwa kwa kiwango Cha lami.

Akizungumza katika mkutano huo Meneja mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande Cha Dar es salaam - Morogoro kutoka TRC,Mhandisi Mbasa amesema kuwa Mradi wa Reli ya Kisasa ni wa maendeleo na wa kimkakati hivyo haukosi changamoto.

Amewataka wakazi wa Kipawa kuwa wavumilivu wakati wakiendelea kuzitatua changamoto hizo. Ameongeza kuwa Pamoja na changamoto za kufanya Tathimini mara mbili maeneo yaliyofanyiwa tathimini ili kupisha Ujenzi wa madaraja yatalipwa na tayari nyumba 42 zimeisha ingizwa kwenye utaratibu wa malipo.

Mhandisi Mbasa aliendelea kueleza kuwa Maeneo hayo ni yanayohusisha barabara za Vingunguti - Barakuda, Uwanja wa ndege - Karakata na ile ya Njia panda ya Segerea.

Awali akitoa maneno ya ukaribisho na utangulizi Diwani wa kata ya Kipawa Mhe Aidan kwezi alimshukuru Mhe Mbunge kwa kuwapatia pesa milioni kumi na tatu na Laki nne (13,400,000) toka katika mfuko wa Jimbo ambazo wamezitumia kununua kompyuta mbili kwa kila shule kwa Shule zote tatu za Sekondari zilizo kwenye kata hiyo pamoja na kompyuta mbili kwa ajili ya zahanati ya Kipawa. Kiasi kingine Cha fedha wamekitumia kukarabati sehemu ya mapokezi katika zahanati ya Kipawa. Mhe. Diwani

Amempongeza Mhe Mbunge kwa kuwa karibu nao wakati wote wanapomuhitaji na kuwasaidia kutatua changamoto za kata hiyo. Ameongeza kuwa kwasasa wamemaliza kabisa changamoto ya mfumo was TEHAMA katika Shule za Sekondari bado watahitaji msaada katika shule za msingi hivyo Mbunge asichoke kuwasaidia.
Share To:

Post A Comment: