Tuesday, 12 October 2021

MBISE AKABIDHI VITI 100 MONDULI

 


Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Arusha Hezron Mbise ametoa viti Mia Moja vya Plastiki kwa Jumuiya ya wazazi  wilaya ya Monduli.


Mbise ametoa viti hivyo wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani humo ya kukagua Uhai wa Jumuiya, Miradi ya Jumuiya hiyo pamoja na utekelezaji wa Ilani.


Alisema Jumuiya hiyo inakabiliwa na changamoto ya miradi na ndiyo sababu ametoa vitu hivyo ili vutumike kukodishwa katika hafla mbalimbali ili jumuiya hiyo iweze kujipatia kipato."Lengo langu ni kuona Jumuiya yetu inaimarika kiuchumi naomba mtunze viti hivi ili mjipatie kipato mnakumbuka mwaka jana niliwapa mizinga mia moja ya kisasa ili kuongeza kipato chao hapa Monduli.Nimefurahi kusikia mizinga hiyo kuna mwekezaji mmempa na analipa fedha kwa wakati".Katika ziara hiyo ambayo mwenyekiti huyo aliongozana na wajumbe wa kamati ya utekelezaji ya Jumuiya hiyo mkoa wa Arusha, Mbise alipokea wanachama wapaya wa Jumuiya hiyo 240.Katibu wa Jumuiya hiyo mkoa wa Arusha Ally Balloh aliwataka wananchi wananchi kuendelea kuchanja chanjo ya UVIKO 19 ambayo inatolewa na serikali bure katika maeneo mbalimbali mkoani hapa.


"Jumuiya ya wazazi jukumu letu kubwa ni malezi niwaombe sana mjitokeze kuchanja chanjo hii lakini pia kuhamasisha familia zetu kuchanja".


Mjumbe wa mkutano mkuu wa  Jumuiya ya wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kutoka mkoa wa Arusha  Lilian Ntiro amewataka wazazi na walezi kufundisha watoto wao maadili mema.Pia amewataka wanaume kuacha kuwapiga na kuwatukana wake zao mbele ya watoto kwa sababu inaathiri watoto kisaikolojia.Aidha amewataka wanawake kuacha tabia ya kushika simu za waume zao na kuzipekua kwa sababu zitawasababishia madhara ikiwemo ugomvi,magonjwa ya moyo na sukari"Niwaombe sana wazazi na walenzi wenzengu tusipekue simu za wenzi wetu kwa sababu zitatuletea migogoro kwenye ndoa na familia zetu hali ambayo itasababisha watoto wetu kukosa maadili mema".Alisema watoto wakipata malezi na makuzi bora watakuwa viongozi bora wa taifa la kesho hivyo ni vyema kila mzazi na mlezi akalea watoto wake vizuri ikiwa ni pamoja na kuwaasa vijana kuacha ulevi kupindukia,madawa ya kulevya na kuchora Tatoo ambazo wakati mwingine zinachangia kukosa ajira katika sekta muhimu.Akishukuru mara baada ya kupokea viti hivyo Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo wilaya ya Monduli Sikirari Mollel alisema mradi huo wa viti wautumia kikamilifu kwa kuvikodisha ili viweze kutupatia kipato cha kuendesha shughuli mbalimbali za Jumuiya yetu.

No comments:

Post a Comment