Na Rhoda Simba, Dodoma 


KATIBU Mkuu wa Umoja wa Vijana wa  Chama Cha mapinduzi (UVCCM) Kenani Kihongosi ametoa rai kwa wanachana na viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kuacha kutoa kauli za uchochezi za kuishinikiza mahakama kumuachia kwenyekiti wao Taifa Freman Mbowe anayeshikiliwa kwa kesi ya ugaidi kuachiwa.


Sambamba na hilo amemtaka Katibu  mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA  kuacha kufanya propaganda za kitoto zilizopitwa na wakati kwani wanacho kifanya ni kuingilia uhuru wa mahakama. 


Akiongea leo na waandishi wa habari jijini hapa katibu huyo amewataka wanachama hao kutambua kuwa Nchi ya Tanzania inaongozwa kwa sheria na taratibu hivyo wanachama na viongozi wa CHADEMA kuacha kuiingilia uhuru wa Mahakama


"Wenzetu hawa wa chama pinzani wamekuwa wakitoa kauli za kuitaka mahakama kumuachia kuongozi wa huyo hivyo tunapenda kwaambia wenzetu hawa mahakam haingiliwi waiache ifanye kazo yake ya utohaji wa haki kama kweli kiongozi huyo ameonewa au tuhuma hizo ni zakweli mahakam itatoa taarifa,"amesema Kihongosi.


Aidha wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha analeta maendeleo ya nchi huku wakimpongeza Rais wa Serikali ya mapinduzi Zanzibar Hussen Ally Mwinyi kwa pamoja kwakuhakikisha wanatekeleza vyema ilani ya chama cha Mapinduzi CCM kwa kuleta miradi mbalimbali ya kimaendeleo.


Hata hivyo wameemdelea kumpongeza Rais Samia kwa kutoa ajira 5000 kwa vijana hapa nchini ambapo ameeleza kuwa serikali imetoa ajira hizo kwa vijana lengo likiwa ni kwenda kulitumikia taifa la Tanzania. 


Mwishoo

Share To:

Post A Comment: