Mkurugenzi wa Habari na Uraghibishi kutoka Tume ya Kudhibiti na Kupambana na Ukimwi (TACAIDS), Bw. Jumanne Issango akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 10, 2021 Jijini Dodoma kuhusu uzinduzi wa Programu ya ONGEA inayotarajiwa kuzinduliwa kesho Septemba 11. 2021.


Sehemu ya Washiriki wakimsikiliza Mkurugenzi wa Habari na Uraghibishi kutoka Tume ya Kudhibiti na Kupambana na Ukimwi (TACAIDS), Bw. Jumanne Issango (hayupo pichani) wakati wa mkutano na waandishi wa Habari kuhusu uzinduzi wa Programu ya ONGEA.
Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto na Wananwake (UNICEF), Bi. Ulrike Gilbert (kushoto) akieleza jambo wakati wa mkutano huo uliowakutanisha na waandishi wa habari katika Ukumbi wa mikutano uliopo Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Septemba 10, 2021 Jijini Dodoma.

 

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama anatarajiwa kuzindua Progamu ya ONGEA kesho Septemba 11, 2021 Jijini Dodoma yenye lengo la kuwajengea uelewa vijana katika kuepuka maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi.

Hayo yalisemwa Mkurugenzi wa Habari na Uraghibishi kutoka Tume ya Kudhibiti na Kupambana na Ukimwi (TACAIDS), Bw. Jumanne Issango wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema Programu hiyo ya ONGEA ni kampeni ambayo imetengeneza vipindi maalum vya redio ambavyo vinaujumbe unaowalenga vijana ili kuwezesha kundi hilo kutambua masuala VVU na Ukimwi.

“Maambuki mapya katika kundi la vijana yamekuwa yakiongezeka kwa hiyo kuzinduliwa kwa programu hii ya ONGEA itasaidia kutoa elimu na kupeleka ujumbe mahusus kwa vijana kuhusiana na masuala ya maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi,” alieleza

Aliongeza kuwa TACAIDS katika kuzindua programu hiyo inashirikiana kwa karibu na wadau wa maendeleo ikiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto na Wananwake (UNICEF), na vyombo vya Habari kupitia Clouds FM na East Africa Radio ambapo vipindi mbalimbali vitakuwa vikirushwa.

Aidha amewahimiza vijana kushiriki kwa wingi katika uzinduzi huo kwani ndiyo walengwa wakubwa pamoja na wakazi wote wa Dodoma akisema nia ya Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ni kuona kijana anatimiza malengo yake na kumuepusha katika mazingira ambayo ni hatarishi.

 

Share To:

Post A Comment: