Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho,akizungumza wakati akifungua maadhimisho ya 18 ya siku ya wahandisi nchini yaliyofanyika leo September 2,2021 jijini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Malongo, akisisitiza jambo kwa wahandisi (hawap pichani), wakati wa maadhimisho ya 18 ya Siku ya Wahandisi, yaliyofanyika leo September 2,2021 jijini Dodoma.


Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), Prof. Ninatubu Lema, akizungumza na wahandisi (hawapo pichani), katika maadhimisho ya 18 ya Siku ya Wahandisi, yaliyofanyika leo September 2,2021 jijini Dodoma.


Msajili wa Bodi ya Wahandisi Patric Barozi,akizungumza katika maadhimisho ya 18 ya Siku ya Wahandisi, yaliyofanyika leo September 2,2021 jijini Dodoma.


Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka ,akizungumza katika maadhimisho ya 18 ya Siku ya Wahandisi, yaliyofanyika leo September 2,2021 jijini Dodoma.


Sehemu ya wahandisi wakifatilia hotuba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho,(hayupo pichani) wakati akifungua maadhimisho ya 18 ya siku ya wahandisi nchini yaliyofanyika leo September 2,2021 jijini Dodoma.


Wahandisi 632 wakila kiapo cha utii katika maadhimisho ya 18 ya Siku ya Wahandisi,yaliyofanyika leo September 2,2021 jijini Dodoma.


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho, akimkabidhi leseni ya uhandisi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Eng. Robert Gabriel, mara baada ya kula kiapo cha utii katika maadhimisho ya 18 ya Siku ya Wahandisi, yaliyofanyika leo September 2,2021 jijini Dodoma.


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB) mara baada ya kufungua maadhimisho ya 18 ya Siku ya Wahandisi,yaliyofanyika leo September 2,2021 jijini Dodoma.

........................................................................................

Na.Alex Sonna,Dodoma

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi,Mhandisi Dk.Leonard Chamuriho amewataka wahandisi nchini kufanya kazi kwa weledi na uadilifu ili kuweza kukamilisha miradi yote nchini kwa muda uliopangwa.

Hayo ameyasema leo September 2,2021 jijini Dodoma wakati akifungua maadhimisho ya 18 ya siku ya wahandisi nchini ambapo jumla ya Wahandisi 3500 wamehudhiria huku Wahandisi 630 wakila kiapo.

Dkt.Chimuriho amesema katika mwaka huu wa fedha serikali imetenga kiasi cha Sh. Trilioni 13.3 kwa ajili ya kukamilisha miradi mikubwa mbalimbali ya Ujenzi inayoendelea na ambayo haijaanza hapa nchini.

''Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais, Samia Suluhu Hassan ameelekeza fedha zitengwa ili kuwezesha miradi mikubwa yote iliyoanza kutekelezwa kukamilika na ambayo ilikuwa haijanza ikamilike''amesema Dkt.Chimuriho

Hata hivyo amesema kuwa kipengele chenye takwa la kisheria la kuwajengea uwezo wahandisi wazawa hususani vijana kiwekwe katika mikataba yote ya ujenzi itakayoingiwa na Serikali kuanzia sasa.

"Ujuzi wakiupata utabaki nchini na utawawezesha wahandisi wetu kuwa na uwezo wa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo hapa nchini, hivyo nawaagiza mhakikishe zabuni zote mpya mtakazo ingia na kuzitoa kwa wakandarasi kigezo cha Kujenga uwezo kiwe cha kisheria''ameongeza

Katika utekelezaji wa miradi kwa 'Force Account' ambao umekuwa ukisababisha wakandarasi binafsi kukosa kazi, amesema kuwa serikali imeiona na tayari imeanza kulifanyia kazi changamoto hiyo kama alivyoelekeza na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kuanzia mradi wa Ujenzi wa mji wa serikali utajengwa kwa ubia na sekta binafsi.

Kwa upande wake Msajili wa Bodi ya Wahandisi Patric Barozi, amesema kuwa mpaka sasa bodi hiyo imesajili jumla ya Wahandisi 31,729 wanawake wakiwa ni 544 sawa na asilimia 32, na kuendeleza Wahandisi 9,441 kati yao wanawake 756, kupitia mpango wao wa kuendeleza wahandisi nchini ambao wamesajiliwa kwenye bodi hiyo kwa mwaka 2020.

Awali Mwenyekiti wa Bodi ya wahandisi, Prof. Ninatubu Lema, aliwataka Wahandisi kwenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia na kujiandaa kukabiliana nayo katika utendaji kazi zao.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka ameeleza kuwa bado kuna shida katika utekelezaji wa miradi mbalimbali inayofanywa na wakandarasi wazawa akiwataka wakandarasi wazawa wanaoshinda zabuni kujenga uaminifu ili waweze kuaminika zaidi na kupewa kazi.

Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Malongo, ameitaka ERB kufanya tathimini ya maazimio yaliyofikiwa mwaka jana kuona kama yametekelezwa na hivyo kujipima katika yale matarajio yaliyofikiwa.

''Umuhimu wa kufuatilia wahandisi wahitimu wanaofanya vizuri katika masomo yao ili kuona kama wanafanya vizuri katika utendaji wa kazi zao kama ambavyo maadili ya taaluma yao yanavyowataka''amesema Mhandisi Malongo
Share To:

JOHN BUKUKU

Post A Comment: