Na Lucas Myovela_ Kilimanjaro

BAADHI ya viongozi na wananchi kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini wamesema kuwa wataendelea kumkumbuka  aliyekuwa mdhamini na mjumbe wa halimashauri kuu ya Taifa ya Chama cha Tanzania Labour(TLP)Marehemu Rose Mrema kwa  kwa ushauri wake na busara zake wakati wa kampeni na harakati za kisiasa katika kipindi cha uhai wake.

Marehemu Rose Mrema aliyekuwa mke wa Mwenyekiti wa Taifa wa TLP,Augustino Mrema  alifariki tarehe 16 mwezi huu katika hospitali ya taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu kutokana na tatizo la shinikizo  la damu alipokuwa akipatiwa matibabu na kuzikwa jana tarehe 21 nyumbani kwake Kiraracha Wilaya ya Moshi vijijini Mkoani hapa

Mkuu wa Mkoa wa Manyara,Mhe,Makongoro Nyerere,alisema kuwa atamkumbuka sana marehemu Rose katika harakati zake za kisiasa katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi hapa nchini mwaka 1995,wakati mume wake akigombea  Urais kupitia Chama Cha NCCR-Mageuzi .

“Nakumbuka kipindi hicho nilipata fursa ya kuzunguka nchi nzima kwa ajili ya kampeni nikiwa na mgombea urais pamoja na marehemu ambapo ndipo nilipoanza kujifunza siasa kwa udani zaidi kwani marehemu alikuwa akiendesha siasa za ustarahabu zisizokuwa na chuki na uhasama”alisema Makongoro Nyeree.

Nyerere aliongeza kuwa Taifa limepata pigo kubwa sana kwani tangu Augustino Mrema kushika madaraka ya kuwa Naibu Waziri mkuu,waziri wa Mambo ya ndani ya Mbunge katika Majimbo mbalimbali hapa Nchini kwa vipindi tofauti  hakukuwahi kutokea na malumbano wala majibizano kati ya serikali na wananchi na hiyo yote ni kutokana na busara zake marehemu.

Akitoa salamu za pole kwa niaba ya wananchi wa jimbo la Vunjo,Mbunge wa  Jimbo hilo Dkt.Charles Kimei(CCM),alisema kuwa marehemu atakumbukwa kwa jitihada zake katika kuhakikisha kuwa kina mama,vijana na wasiojiweza wakiwemo walemavu ndani ya jimbo hilo wanajikwamua kiuchumi.

“Marehemu  alikuwa anawapa mikopo nafuu ambayo ilikuwa aikiwasaidia kuanzisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi pamoja na kuondokana na umasikini,ambapo pia aliwasaidia vijana kupata elimu pamoja na misaada mbalimbali kwa makundi ya wasiojiweza.”alisema Mbunge huyo.


Dkt.Kimei alisema kuwa  jamii inatakiwa kumkumbuka marehemu kwa kutambua mchango wake alioutoa jimboni hapo na kuwataka wanawake wengine kuiga mfano wa marehemu Rose mrema kwani mbali na Siasa pamoja na michango yake ya kimaendeleo jimboni hapo alikuwa akimkumbuka Mungu wakati wote kwani alishiriki katika shuguli mbalimbali ya kidini ikiwemo ujenzi wa nyumba  za ibada pasipo kujali itikadi ya kidini.

Kwa upande wake mume wa marehemu,Augustino Mrema alisema kuwa akilia atakuwa anamkufuru mungu kwani ameishi naye katika ndoa kwa miaka 48,hiyo hata akilia aitomsaidia chochote kwani hata angepewa miaka zaidi ya hiyo ni lazima angekufa kama maandiko yasemavyo kila nafsi lazima itaonya mauti.

“Mke wangu Rose ni kama aliona kifo chake kwani hivi karibuni aliikutanisha familia yake yote na kuipa nasaa ambapo alisisitiza waishi kwa amani na upendo huku wakijikita zaidi akatika kusaidia makundi yenye uhitadi katika jamii na kumtanguliza mungu.hivyo wanangu wasiponiangalia kama alivyokuwa akiniangalia mama yao watakuwa wamekiuka wosia wa marehemu mke wangu”alisema Mrema.

Akiongoza sala ya mazishi Paroko wa Parokia ya Uomboni Marangu,jimbo Katoliki la moshi,Padri Adelard Imani  alisema kuwa wamempoteza msharika wa muhimu sana kwani alikuwa miongoni mwa watu ambao walikuwa wakisaidia kanisa na jamii kwa ujumla hivyo watamkumbuka na wao kama parokia watazidi kumuombea apumzike kwa amani.

Marehemu Rose Mrema alizaliwa mwaka tarehe 5 mwezi 1 mwaka 1954 huko Marangu mkoani hapa ambapo ameacha mume,watoto sita na wajukuu kumi na tatu.

BWANA MOTOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIIMIDIWE.


Share To:

Lucas Myovela

Post A Comment: