Na Asila Twaha - Dodoma


Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Elirehema Kaaya amesema Uchaguzi wa viongozi wa ALAT, utafanyika kuanzia tarehe kuanzaia 27 hadi 29 Septemba, 2021, ambapo pamoja na mambo mengine Mkutano huo utabebwa na ajenda kuu yakuwapata viongozi wake watakao hudumu kwa muda wa miaka mitano.


Akiongea na waandishi wa habari mapema leo Septemba 13, 2021 Jijini Dodoma   Kaaya amesema, mpaka sasa maandalizi ya mkutano huo yamekamilika huku akiwahimiza wajumbe halali wa Mkutano huo kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za jumuiya hiyo ikiwepo ya mwenyekiti wa taifa, makamu mwenyekiti, pamoja na wajumbe wa kamati tendaji.


Uchaguzi wa Viongozi wa ALAT ni kwa mujibu wa katiba ya Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), ambapo  ndani ya katiba wanatakiwa kila baada ya miaka mitano wafanye uchauzi baada ya upatikanaji wa uundaji wa baraza la madiwani na upatikanaji wa viongozi ALAT kwa ngazi ya Mkoa.


“Ifahamike kwamba, Mkutano huo utawaleta kwa pamoja Mameya, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmashauri za majiji, manispaa, miji pamoja na halmashauri za wilaya” Amesema Kaaya.


Kaaya amefafanua kuwa, Mkutano huo, unatazamiwa kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.


Kufanyika kwa Mkutano Mkuu Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Dodoma ni fursa la Baraza la Madiwani wa Mkoa wa Dodoma, kushiriki pamoja na Makatibu Tawala wasaidizi wanaoshughulika na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Share To:

Post A Comment: