****************************

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetoa mafunzo kwa Wajasiriamali na Wasindikaji wa korosho mkoani Mtwara ili kuwajengea uelewa kuhusu viwango katika bidhaa zao.

Akizungumza mara baada ya kufungua mafunzo hayo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesema wajasiriamali na wasindikaji wa korosho wasiopungua 40, wanapatiwa mafunzo kwani wanafanya shughuli zao na tayari bidhaa zao zipo kwenye soko ila hazijathibitishwa ubora na TBS.

Aidha amesema mafunzo hayo ni njia muafaka wa kuleta tija zaidi katika juhudi za kuliletea taifa maendeleo ya haraka kulingana na fursa zilizopo hasa kwenye sekta ya viwanda,Kilimo,Biashara, Uvuvi na maeneo mengine mengi.

"Mafunzo haya yamekuja kwa wakati muafaka ambapo Serikali imeazimia kwa dhati kabisa kuendeleza viwango ili kutoa ajira katika kada mbalimbali pamoja na kuziwezesha bidhaa zetu kushindana katika masoko ya ndani, kikanda na nje ya nchi". Amesema Mhe.Brigedia Jenerali Gaguti.

Amesema TBS inaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na watendaji waliopo katika halmashauri zetu nchini ili kurahisisha kufikisha huduma kwa wananchi.
Share To:

JOHN BUKUKU

Post A Comment: