Wednesday, 1 September 2021

TANESCO KAGERA YATEKELEZA AGIZO LA NAIBU WAZIRI BYABATO

 Shirika la Umeme Nchini Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Kagera wameendelea na jitihada za kusogeza Huduma ya Umeme karibu na Wananchi na wateja wao ambao hawakuwahi kupata Umeme huo tangu kuumbwa kwa Dunia.

Hivi karibuni Naibu Waziri Nishati Mhe Stephen Byabato Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini,  amewasha umeme kwenye Nyumba ya Mama Ajuna Mkazi wa Maeneo ya Kagondo Kaluguru -Mjimwema mtaa waomkigere Ikiwa ni kuashiria kufikishwa kwa huduma ya umeme Kwenye eneo Hilo ambalo halikuwahi kuwa na Umeme kabisa.

Akizungumzaa na wakazi wa Mtaa Kagondo wakati wa Tukio hilo, Mhe. Byabato amewapongeza TANESCO Kagera kwa kufikisha umeme eneo Hilo Ndani ya Muda aliowapa, zaidi Mhe Byabato Alisema ataendelea kufuatilia na kuhakikisha TANESCO wanatekeleza agizo lake la kufikisha umeme Maeneo mengine yasiyo na Umeme Ndani ya ukanda wa Kijani (Green Belt)na  Bukoba Manispaa kwa ujumla yapate huduma ya umeme ifikapo Novemba 2021.

Akishukuru kwa Niaba ya Wakazi wa Mtaa huo, Mama Ajuna ambaye Nyumba yake ndipo lilipofanyika Tukio la kuwashwa kwa Umeme huo aliwashiwa umeme Kwenye nyumba yake, ameipongeza kazi kubwa iliyofanywa na Serikali kupitia Tanesco  kumfikishia huduma ya umeme ambayo alikua akiisubiri kwa Muda mrefu.
 

No comments:

Post a Comment