Naibu Waziri Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga akikagua maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mfano inayojengwa Iyumbu jijini Dodoma.
Muonekano wa hatua za Mabweni ya Wavulana katika Shule ya Sekondari ya Mfano inayojengwa katika eneo la Iyumbu jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mfano Iyumbu jijini Dodoma leo


Naibu Waziri Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga akizungumza na wandishi wa habari baada ya kumaliza kukagua ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mfano Iyumbu jijini Dodoma na ujenzi wa Chuo cha Ufundi Nala.


Charles James


SERIKALI imeagiza Shule ya mfano ya Iyumbu ambayo itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi takribani 1,000 ikamilike Desemba mwaka huu.

Kauli hiyo ili imetolewa na Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia, Omar Kipanga wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa Shule ya Mfano iliyopo Iyumbu na ujenzi wa Chuo cha Ufundi cha Dodoma kilichopo Nala Lugala Jijini Dodoma.

Naibu Waziri huyo amesema katika eneo la Iyumbu Serikali inajengwa Shule ya mfano kwa gharama ya Sh bilioni 17.1 .

Amesema ujenzi huo ni kielelezo kuwa Serikali inawajali wananchi wake na kutoa kipaumbele katika suala la elimu.

Amesema awali Shule hiyo ilipangwa kukamilika Februari mkwaka 2022 lakini ameagiza Shule hiyo ikamilike Desemba Ili ifikapo Januari mwakani ianze kuchukua wanafunzi wa Sekondari. "Naagiza ujenzi ikamilike Desemba Ili Januari wanafunzi wadahiliwe kea ajili ya kuanza masomo," Amesema.

Amesema tangu Serikali ilipopitisha utaratibu wa elimu.bila malipo kuna idaho kubwa ya wanafunzi wanaopata fursa ya kuandikishwa Shule na hivyo kuongeza mahitaji ya shule na vyumba vya madarasa.

Akitoa taarifa ya Ujenzi kwa Naibu Waziri, Naibu Kamanda wa Operesheni wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Geoffrey Ngole amesema ujenzi ulianza July 2020 na utakamilika Februari mwaka 2022.

"Tumepokea maagizo ya Naibu Waziri ya kukamilika Kazi ifikapo Desemba, turaongeza nguvu Kazi na tutafanya Kazi usiku na mchana Ili tumalize kwa muda uliotajwa na Naibu Waziri," Amesema.

Amesema ujenzi huo uko katika sehemu tano ikiwemo jengo Kuu, bweni la wasichana lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 500 na bweni la wavulana lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 500, bwalo, nyumba 10 za Watumishi,jengo la Utawala, Nyumba za Walimu, Viwanja vya michezo na matanki ya maji.

Pia Naibu Waziri Kipanga amesema Serikali imetimiza azma yake na Chuo hicho kitakapokamilka kitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 3,000 ambapo awamu ya kwanza kitachukua wanafunzi 1,500.

Amesema Serikali imetoa Sh bilioni 17.9 na Kazi ya Ujenzi ikianza Juni 19 Mwaka huu na itachua miezi 18. Amesema lengo la Chuo hicho ni kuwezesha vijana wengi kupata ujuzi, kuzalisha vijana wenye ujuzi wa kati.

Amesema Serikali imejipanga kujenga Vyuo vya Ufundi katika kanda zote ikiwemo kanda ya Kati, kanda ya ziwa, kanda ya Kusini na kanda ya kaskazini.

Kwa upande kwake, Mhandisi Msaidizi kutoka Kampuni ya BICO, Aliki Nziku amesema mradi huo mpango wa Serikali kuongeza Wataalam katika nyanja za ufundi na Teknolojia maabara.

Amesema mradi huo unajengwa na Mkandarasi CRJE limited kwa gharama ya Sh bilioni 17.9 chini ya usimamizi wa washauri waandamizi wa BICO.


Share To:

Post A Comment: