MBUNGE wa Viti Maalumu CCM kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Mhe Neema Lugangira 
 

MBUNGE wa Viti Maalumu CCM kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Mhe Neema Lugangira amesema hatua ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhudhuria Mkutanowa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, New York nchini Marekani na kulihutubia Baraza hilo itasaidia kufungua fursa nyingi na kuwaweka Watanzania katika nafasi nzuri ya kunufaika 


Mbunge Neema Lugangira aliyasema hayo leo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ambapo alisema kwa sababu Rais Samia Suluhu anapokwenda kuhudhuria Mkutano huo mkubwa wa Umoja wa Mataifa anakutana na fursa nyingi na mahitaji duniani yapo mengi na ushindani ni mkubwa sana baina ya nchi na nchi hivyo kitendo cha kushiriki kwenye mkutano huo kitafungua milango kwa Tanzania na kuiweka Tanzania katika nafasi ya kupata kipaumbele kwenye fursa mbalimbali.

Alisema kwa sababu Rais Samia amepanga kuwa na mikutano mengine mingi ikiwemo kukutana na wakuu wa Taasisi za Kimataifa na Marais wa Nchi nyengine na kushiriki katika kilele cha mikutano mengine inayohusu Usalama wa Chakula, Mabadiliko ya Tabia Nchi,  na Utekelezaji waMalengo ya maendeleo Endelevu (SDGs)...."Hivyo nikiwa kama Mbunge na Mwenyekiti wa Wabunge Vinara wa Usalama wa Chakula nimefarijika kuona Mhe Rais ameibaba agenda yetu ya Usalama waChakula hivyo tunasubiri kwa hamu kusikiliza hotuba yake na kutekeleza aliyokubaliana na Umoja wa Mataifa na Wadau wengine.

Aidha, Mbunge Lugangira aliwataka Watanzania wakae tayari na kuchangamkia fursa zitakazotokana na ziara hiyo ya Mhe Rais Samia ambayo itakuwa chachu kwa chachu Maendeleo ya Taifa.

“Kwa kweli nimefurahi sana kwa kwa sababu Mhe Rais Samia Suluhu Hassan anakwenda kuhudhuria
Mkutano Mkuu wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na atahutubia kwenye baraza hilo. Ni jambo kubwa sana na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan anastahili pongezi kubwa kwa uamuzi wa kushiriki maana mara ya mwisho Rais wa Tanzania kushiriki mkutano wa Mwaka wa  Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ilikuwa ni 2015". 

Mbunge Lugangira alitoa areja mwaka 2019 Tanzania ilifanya tathimini ya utekelezaji wake wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (Sustainable Development Goals- SDGs) na katika tathimini hiyo ilionyesha Tanzania haifanyi vizuri katika lengo la namba 17 (SDG 17) ambayo inalenga mashirikiano na mahusiano baina ya nchi moja na nchi
nyengine na wadau wengine kama Sekta Binafsi, Asasi za Kiraia na Wadau wa maendeleo. Alisema hivyo ilishauriwa Tanzania iweke jitihada kubwa kuhakikisha inaimarisha mahusiano yake na ushirikino wake ili iweze kutekeza lengonamba 17 (SDG 17).

“Watanzania mtakubaliana nani kwamba tokea Mhe Rais Samia ameingia Madarakani hiyo agenda ya SDG 17 kuhakikisha Tanzania inaimarisha mahusiano na ushirikiano  wake na Mataifa mengine,  Sekta Binafsi, Asasi za Kiraia, na Wadau wa Maendeleo ameibeba na imekuwa ni moja ya agenda zake kuu.

Mbunge huyo alisema hivyo Mhe Rais Samia amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha Tanzania inaimarisha mahusiano na mashirikiano na tayari Mhe Rais Samia anatekeleza yale yaliyo shauriwa kwenye tathmini ya mwaka 2019.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: