Taasisi za Benki ya Stanbic Tanzania na Shule Direct zimeunga mkono jitihada za kuboresha mazingira ya kusoma kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mbabala-Dodoma jiji kwa kugawa viti na meza 100 pamoja na seti ya Kompyuta na Printer kwa uratibu wa shughuli za ofisi na uchapaji wa mitihani.


Akipokea msaada huo,Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mh Jabir Shekimweri ameishukuru Benki ya Stanbic kwa kuchangia viti na meza na kuwaomba wadau wengi zaidi kujitokeza kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha mazingira ya wanafunzi kusoma.


Naye Mbunge wa Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde ameeleza kuwa mchango huo wa viti na meza utasaidia kupunguza changamoto za upungufu wa viti na meza shuleni hapo na kutumia fursa hiyo kuiomba Benki kuifanya Shule hiyo kuwa ya mfano ya mradi wa kugharamia Elimu unaotekelezwa chini ya uangalizi wa benki hiyo.


Akitoa maelezo yake,Mkurugenzi wa Huduma za kibenki wa Benki ya Stanbic Ndg. Omar Mtiga amesema ni dhamira ya Benki kuhakikisha inashirikiana na serikali katika kutatua changamoto za sekta ya elimu kwa kuja na mpango kabambe wa kusambaza madawati nchini na utunzaji wa mazingira ambapo katika kila dawati moja wanalotoa wanahakikisha pia wanapanda mti mmoja.Mpango huu umeanzia Katika Shule ya Sekondari Mbabala Dodoma ambapo jumla ya viti na meza vyenye thamani ya Tsh 12,000,000 vimetolewa.


Katika kuunga mkono matumizi ya Teknolojia katika Shule za Sekondari,Taasisi ya Shule Direct kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji wake Bi. Faraja Kotta Nyalandu imeahidi kutoa seti ya Kompyuta na Printer kuuitikia wito wa Mbunge Mavunde ambaye aliwasilisha ombi hilo rasmi.

Share To:

Post A Comment: