Monday, 16 August 2021

Waziri Ummy awanyooshea Kidole Sengerema Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo

 


Nteghenjwa Hosseah, Sengerema 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Ummy Mwalimu amewanyooshea Kidole Uongozi wa Halmashauri ya Sengerema kwa kwashindwa kuweka vipaumbele kwenye Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.


Waziri Ummy akiwa ziarani Wilayani Sengerama mapema Tarehe 14.08.2021 alibaini baadhi ya changamoto kwenye maeneo mbalimbali ambayo kama Halmashauri wangeweka vipaumbele changamoto hizo zingeshatatuliwa.


Waziri Ummy alitembelea Shule ya Msingi Sengerema iliyopo Kata ya Nyampulikano kukagua matundu ya vyoo ambayo ni chakavu kwa muda mrefu na pia sio salama kwa wanafunzi pamoja na Shule ya Msingi Isome ambapo alijionea namna watoto wanavyosomea kwenye vyumba ambavyo havina Sakafu na uhaba wa madawati.


Alihoji Watumishi wa Halmashauri hiyo kwanini changamoto za namna hiyo ambazo zinagharimu fedha ndogo tu hazijatatuliwa kwa muda mrefu ilihali Halmashauri inakusanya mapato ya kutosha.


“Changamoto ninayoiona hapa Viongozi wa Halmashauri hamna vipaumbele maana kuweka sakafu darasa moja haiwezi kuzidi hata Laki sita ina maana halmashauri mmeshindwa na kuacha watoto wasome kwenye darasa lenye vumbi namna hii na wakae chini kwa kukosa dawati wakati dawati moja ni shilingi elfu hamsini tu? Alihoji Waziri Ummy


Sasa niwapa maelekezo nataka kuona changamoto hizi za Wanafunzi zinatatuliwa haraka na muweka vipaumbele katika kutatua changamoto za Wananchi sitaki kuona vitu vidogo vidogo kama hivi vinaripotiwa kila wakati wakati vipo ndani ya uwezo wenu” Alisisitiza Mhe. Ummy

No comments:

Post a Comment