Na Karama Kenyunko,


MWENYEKITI wa Chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia anaiomba Serikali wakae meza ya maridhiano kwa ajili ya kumaliza kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Mbatia ameyasema hayo leo Agosti 6,2021 nje ya viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa na kusomewa mashtaka upya kwa kuunganishwa na wenzake watatu

Akizungumza mara baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, Mbatia amesema kinachoendelea kwa sasa (kesi) hakileti afya kwa Taifa na kwenye nyanja mbali mbali ikiwemo Kiuchumi na Kijamii.

"Wakati kesi inaendelea ninaiomba serikali tukae meza ya maridhiano kwa ajili ya kumaliza kesi hii", amesema Mbatia

Aidha amesema, ataongeza jopo la mawakili wanne kutoka kwenye chama chake ambao watasaidiana na mawakili tisa waliopo kwenye kesi hiyo wakiongozwa na Peter Kibatala kwa ajili  ya kumaliza kesi hiyo na kwamba tayari wameishakubaliana na kibatala kufanya hivyo.

Mbali na Mbowe washtakiwa wengine ni  Halfan Hassan, Adam Kasekwa na Mohamed Lingwenya.

Washtakiwa wote wanakabiliwa na shtaka la kula njama ya kulipua vituo vya mafuta na mikusanyiko ya Umma. Huku Mbowe peke yake akikabiliwa na shtaka la kufadhili vitendo vya kigaidi, na washtakiwa Hassan, Kasekwa Lingwenya wakidaiwa kupokea pesa kutoka kwa Mbowe kwa ajili ya kufanya vitendo vya kigaidi.

Pia mshtakiwa Kasweka anadaiwa kukutwa na silaha aina pisto na risasi tatu huku mshtakiwa Hassan akikutwa akitumia sare na vifaa vya jeshi.Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 13,2021 itakapokuja kwa ajili ya washtakiwa kusomew maelezo ya mashaidi (Committal
Share To:

Post A Comment: