Tuesday, 27 July 2021

WAZIRI WA AFYA AKUTANA NA MKURUGENZI WA SHIRIKA LA KUPAMBANA NA MAGONJWA AFRIKA {CDC} JIJINI DAR ES SALAAM.


 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima leo amekutana na Mkurugenzi kutoka Shirika la kupambana na magonjwa Afrika CDC Dkt. John Nkengasong aliyeambatana na wenzake Dkt. Djoudallayo Benjamin na Dkt. Theresa Madubuko.

Kikao hicho kimefanyika leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Jijini Dar es Salaam, kimehudhuriwa pia na Wataalamu kutoka Wizara ya Afya na Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiongozwa na Dkt. Leonard Subi.

Katika kikao hicho kwa pamoja wamekubaliana kushirikiana na kubadilishana uzoefu katika kupambana na magonjwa mbali mbali ikiwemo maambukizi ya wimbi la tatu la ugonjwa wa Corona ili kuutokomeza nchini.

 No comments:

Post a Comment