Na. Angela Msimbira KIGOMA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mika na Serikali za Mitaa  Mhe Ummy Mwalimu amezitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha  wanatumia Mifumo ya kielekroniki katika ukusanyaji wa Mapato ya ndani ya Halmashauri na kupelekwa benki ndani ya masaa 24


Akiongea na Sekretarieti ya Mkoa wa Kigoma  leo kwenye ziara ya kufuatilia shughuli za maendeleo  katika mkoa huo katika Sekta ya Afya ya msingi, maendeleo ya shule za msingi na Sekondari, mundombinu  ya barabara na ukusanyaji wa mapato ya ndani  na matumizi ya Halmashauri.


Waziri Ummy amaeendelea kufafanua kuwa kila Halmashauri inawajibu wakuhakikisha wanatumia mifumo hiyo katika ukusanyaji wa mapato ya ndani ili kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha katika Halmashauri.


Ameendelea kufafanua kuwa  Halmashauri zinatakiwa kuhakikisha mapato yanayokusanywa na Halmashauri  yanaingizwa benki  ndani  ya masaa 24 kwa kuwa kati ya Halmashauri 8 za Mkoa wa Kigoma, Halmashauri 6 zimepata hati zenye mashaka  na Halmashauri 2 zimepata hati za kuridhisha  katika mwaka 2019/2020 sababu kubwa ni fedha kukusanywa na kupelekwa kwa wakati benki.


Amezitaja Halmashauri ambazo zilikusanya fedha na kutokuzipeleka benki kwa wakati lakini kwenye mfumo yanaonekana kuwa ni Halmashauri ya Wilaya ya  Kigoma ambapo haikupeleka kiasi cha shilingi milioni 378, Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu milioni 112 , Halmashauri ya Buhighwe  milioni  74 na Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo 430 na Halmashauri ya Wilaya wa uvinza shilingi milioni 318.


Amewataka Viongozi wa Mkoa na Wilaya kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa mapato ya ndani na kuhakikisha fedha zinazokusanywa  zinapelekwa  benki kwa wakati.


Aidha, amewaagiza viongozi hao kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri na yanatumika  katika kutatua kero za wananchi  ambapo kila shilingi 100 inayokusanywa  shilingi arobaini inatengwa kwa ajili ya kutatua kero za wananchi wa Kigoma.

Share To:

Post A Comment: