Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Philemon Sengati akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo.

 

WAZIRI mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, ana tarajiwa kuwa mgeni Rasmi kwenye maonesho ya biashara ya Teknolojia na Madini mkoani Shinyanga.

Maonesho hayo yatafanyika kuanzia Julai 23 mwaka huu hadi Agost Mosi, katika viwanja vya Butulwa, Kata ya Old Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Philemon Sengati, amebainisha  hayo leo wakati akizungumza na vyombo vya habari ,kuwa maonesho hayo ni ya awamu ya pili, ambayo yamelenga kukuza Sekta ya Madini na biashara mkoani humo.

Alisema Mkoa wa Shinyanga una migodi mingi ya madini , hivyo kupitia maonesho hayo, yatatoa fursa kwa wawekezaji kuja kuwekeza mkoani humo, pamoja na kuunganisha mtandao wa wafanyabiashara.

"Maonesho haya ya Biashara na Teknolojia ya madini mkoani Shinyanga, yatatusaidia kukuza uchumi wa Mkoa wetu, na  pato la mtu mmoja mmoja, na Taifa kwa ujumla, na tuta yafungua Julai 23, na Mgeni Rasmi atakua Waziri Mkuu Kassim Majaliwa," amesema Dk. Sengati.

"Tunaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kwenye maonesho haya, kuja kuona madini live, pamoja na wafanya biashara wajumuike ili wapate mtadao na kukuza biashara zao," ameongeza.

Naye Mwenyekiti wa Maonesho hayo Kulwa Meshack, ambaye ni Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara, viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA)mkoani Shinyanga, alisema maonesho hayo ni fursa kwa wachimbaji na wafanyabiashara, ambapo watabadilisha uzoefu namna ya kufanya kazi zao.

Share To:

Post A Comment: