Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha Zelothe Stephen Zelothe akiwa ameambatana na wenyeviti wa mashina na matawi wakikagua dampo lililopo ndani ya makazi ya watu katika Kitongoji cha Sinon Kusini Wilayani Monduli ambalo limekuwa kero kwa wananchi.
Muonekano wa Dampo hilo lililopo katikakati ya makazi ya wananchi wa Kitongoji cha Sinoni Kusini.

Na: Imma Msumba,Monduli


WAnanchi wa Kitongoji cha Sinoni Kusini katika kata ya Engutoto wilayani Monduli wamemlalamikia Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi Mkoa wa Arusha Zelothe Stephen  kitendo cha  uongozi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kuweka Dampo la taka  katika maeneo ya makazi ya watu na kutishia kutokea kwa ugojwa wa kipindupindu katika msimu wa mvua.
 
Bi. Lucy Laizer mkazi wa kitongoji cha Sinoni Kusini alisema kumewepo  na  usumbufu mkubwa  na badhii ya wakazi wa Kitongoji hicho wenye watoto wadogo huwalazimu kuhama nyumba  kutokana kukidhiri kwa taka katika mtaa na harufu mbaya pamoja na moshi mkali pindi wachomapo taka hizo huwaathiri kiafya  na kusababisha vikohozi kwa watu wa mtaa huo.
 
 Bi. Laizer alisema  baadhi ya wakazi wa kitongoji hicho cha Sinoni Kusini wamekuwa wakiadhiriwa na harufu kali na kutishia wakazi wa kitongoji hicho kupata ugonjwa wa kikohozi wakati halmashauri ikiendelea kuchoma taka katika eneo la korongo ambalo liko katikati ya  makazi ya watu .
 
Aidha Bi laizer alienda mbali na kuulalamikia uongozi wa  halmasahauri kitengo cha usafi na mazingira kwa kusema kuwa wameshidwa kutekeleza na kuendana na kauli ya Serikali ya Awamu ya sita ya kuwataka wanachi kufanya usafi  ili  kuweza  kujikinga na magonjwa yanayoweza kusababishwa na uchafu.
 
Kwa upande wake Diwani wa Kata hiyo ya Engutoto Nelson Ngoyai Lowassa alikiri kuwepo na tatizo hilo katika eneo la kitongoji hicho kuadhiriwa na kadhia hiyo ambapo alisema kuwa takataka nyingi zinatupwa kwenye korongo zinazalishwa  na wafanyabiashara wa sokoni na wakazi wa Mji wa Monduli na kuzitupa katika korongo hilo.
 
Diwani Lowassa alisema suala hilo amelifikisha katika Baraza la madiwani la Halmashauri na tayari eneo limeshapatikana hivyo ndani ya kipindi kifupi dampo hilo litahamishiwa sehemu husika maana tayari Halmashauri imeshapata eneo kwa ajili ya kuweka dampo kubwa na la kisasa.
 

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Monduli Frank James Mwaisumbe akizungumza nasi alikiri kuwepo kwa tatizo hilo nakusema

"Hilo tatizo la jalala nimelikuta,ila mkumbuke ndo kwanza mgeni hapa monduli nina wiki mbili tu sasa hapa,Lakini kama mnavyojua eneo kubwa la wilaya ya monduli limezungukwa na Jeshi maeneo ya ardhi huku ni hafifu sana lakini tunashukuru ndugu zetu wa Jeshi la Wananchi JWTZ wameshatupatia eneo kubwa Sana na tayari tumeanza mchakato wa kutengeza dampo kubwa na la kisasa katika eneo tulilopewa na Jeshi hivyo ndani ya muda mfupi ile adha pale kwa wananchi wa Kitongoji cha Sinoni Kusini itaondoka" Alisema Mwaisumbe Mkuu wa Wilaya

Share To:

Post A Comment: