Na Mwamvua Mwinyi,Kisarawe
NAIBU waziri wa maji ,MaryPrisca Mahundi ameagiza Wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA )Mikoa na wilaya nchini kuacha tabia ya kukumbatia fedha za baadhi ya miradi ya maji ,ili kuwezesha miradi kumalizika kwa wakati .

Aidha ametaka vyanzo vya maji vilindwe huku akielekeza kuchukuliwa hatua kwa watu wanaobainika kuchezea vyanzo vya maji ili iwe fundisho kwa wengine.

MaryPrisca aliyasema hayo katika ziara ya kikazi wilayani Kisarawe ,ambapo aliwataka mameneja wa RUWASA Mkoa na wilaya kutumia fedha wanazopokea kwa wakati pasipo kulala nazo .

"Ipo mikoa ana wilaya ambazo wanalala na fedha Za miradi hali inayosababisha miradi kusuasua na kushindwa kukamilika kwa wakati lengwa "

Naibu Waziri huyo alielezea ,serikali inatoa fedha kidogo kidogo kulingana na mradi na amewahakikishia zitaendelea kupelekwa kwenye maeneo yao .

"Wizara imejipanga na serikali inaendelea kuwaunga mkono ,kwa lengo la kumtua ndoo mama kichwani hivyo sisi kama wasaidizi wake ni vyema kuangalia serikali inayoyaagiza kuona kama yanafanyiwa kazi " alifafanua MaryPrisca.

Pia aliwaasa wataalamu mbalimbali kufanya kazi kwa kushirikiana na viongozi na kuacha kufanya kazi kwa mazoea .

Kwa upande wake meneja wa RUWASA Kisarawe Majid Mtili alieleza RUWASA imejipanga kufikisha maji safi na salama vijijini ili kupunguza kero ya ukosefu wa maji .

Alisema kupitia RUWASA ipo miradi inayoendelea na ujenzi na ukamilishaji wa miradi ya maji ikiwemo mradi wa maji Boga -Mengwa unatekelezwa kwa kutumia wataalamu wa ndani kwa gharama ya sh .milioni 465.254. 1 na milioni 250 zimeshapokelewa na umefikia asilimia 75.

Majid alisema mradi mwingine ni Chole na Kwala sh .milioni 602.559 ujenzi umefikia asilimia 80 na umeanza kutoa huduma kwa watu 4,818 na ukarabati wa mradi wa maji Mafizi milioni 169.609.4 ambapo milioni 77.085.950 zimetumika hadi sasa na mradi umefikia asilimia 35 .

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kisarawe ,Nickson Saimon alisema hali ya upatikanaji wa maji ni asilimia 53 sawa ya watu 49,569 wanaopata huduma ya maji safi .

Alisema wananchi wa vijijini wanapata maji kwa sasa kwa asilimia 65 ambapo vijij 15 vinapata maji ya kutosha ,vijiji 26 maji wastani na vijiji 24 havina maji .

Katika ziara hiyo wamepitia kijji cha Masaki ,Kikwete,Chole na Boga na kesho Naibu wazir huyo anatarajia kutembelea miradi ya Mkuranga.
Share To:

Post A Comment: