BODI
ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (Cereals and Other Produce Board of
Tanzania - CPB), ina mpango wa kutumia Shilingi Billion 2.3 kwenye
ukarabati wa kiwanda cha Unga cha Arusha eneo la Unga Limited katika
mikakati yake ya kukifanya kinaongeza uzalishaji wa unga wa sembe toka
tani 40 mpaka tani 60 kwa siku.
Akiongea
katika mahojiano maalumu ya ufafanuzi kufuatia taarifa potofu kadhaa
zilizotolewa hivi karibuni katika mitandao ya kijamii, Meneja wa
Kiwanda cha Arusha Bw. Hizza amesema tayari mkandarasi wa kufanya
ukarabati huo mkubwa ameshapatikana na kazi inatarajiwa kuanza wakati
wowote ule.
Bw.
Hizza amesema kwamba hatua hiyo ni moja ya mikakati mingi ambayo Bodi
hiyo imepanga kutekeleza katika kuwandolea wakulima tatizo la masoko
pamoja na bei kadhalika na upatikanaji wa mbegu bora na pembejeo ikiwa
ni msimamizi katika ubora ndani ya biashara ya nafaka
Amesema
Bodi hiyo, ambayo ni taasisi ya serikali chini ya wizara ya Kilimo
iliyopewa dhamana ya kufanya biashara ya nafaka na mazao mchanganyiko
chini ya Sheria ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Na.19 ya Mwaka 2009,
tayari imeshaingia mkataba na wakulima wa ngano kwa kusambaza tani 225
za mbegu bora kwa wakulima wa wilaya tano kwenye mikoa ya Kilimanjaro,
Arusha na Manyara katika mwaka wa fedha wa 2020/2021.
Bw.
Hizza ameeleza kwamba mbali ya usambazaji wa mbegu na kuwahakikishia
wakulima soko la ngano, pia CPB imetoa maafisa ugani ambao watakuwa na
wakulima katika kipindi chote cha ukulima wa zao la ngano ili kutoa
elimu na kuhakikisha uandaaji wa mashamba darasa sehemu mbalimbali kwa
wakulima wa ngano.
Amesema
CPB kwa kushirikiana na kampuni ya kuzalisha na kusambaza mbegu ya Seed
Co itatoa elimu na wataalam kwa wakulima kwenye maeneo hayo ili
kuwawezesha kupata mavuno mengi na bora, na kwamba Bodi ilikabidhi mbegu
za ngano ya chakula, zenye ubora wa hali ya juu kutokana na kuwa na
protini ya kutosha.
“Hivyo
ngano itakayovunwa itafaa zaidi kwa matumizi ya nyumbani na viwandani,
ambako hutumika kutengeneza mikate, keki, chapati na vyakula vingine.
“Vilevile
CPB imewahakikishia wakulima wote wa ngano kununua ngano yote baada ya
mavuno ili kuwaondolea wakulima wengi tatizo la masoko pamoja na bei”,
ameongezea.
Bw.
Hizza ameeleza pia kwamba zaidi ya ekali 3,000 za mashamba ya ngano
zimelimwa na wakulima 270 wamesajiliwa na Bodi katika kilimo cha mkataba
cha ngano ambapo msimu huu CPB inatarajia kupata tani 7,000 za ngano
kutoka kwa wakulima kupitia mpango huo.
Bodi
hiyo ina viwanda vilivyopo Mwanza, Arusha, Dodoma na Iringa ambavyo
vyote vilikuwa chini ya umiliki wa shirika la Taifa la Usagaji (NMC).
Kiwanda kilichopo Arusha ambacho kimetajwa kuwa ni mkombozi mkubwa wa
wakulima wa kanda ya kaskazini kinasindika unga wa sembe na ngano pamoja
na kununua nafaka ambapo wakulima wameweza kupata soko la uhakika la
mazao yao.
Wakulima
wengi wa kanda ya Kaskazini wameishukuru CPB kwa hatua zake mbalimbali
inazochukua katika kuimarisha uzalishaji, ununuzi na kuongeza thamani
mazao ya nafaka, wakiitaja kuwa ni mkombozi wao mkubwa katika sekta hio.
Wakiongea
kwa nyakati mbalimbali, wakulima hao wamesema tangu CPB ilipoanza
kutekeleza majukumu yake, ahueni ya kupata soko ya mazao yao imekuwa
kubwa kuliko wakati wowote ule.
“Siku
hizi tunalima kwa amani tukijua kwamba mazao yetu yana soko tayari
tofauti na zamani ilikuwa kama tunalima kwa kucheza pata potea”, amesema
Bw. Amanieli Mwingia, mkulima wa mahindi mkoani Arusha, baada ya
kupokea malipo ya mazao aliyoiuzia bodi mwaka huu.
Bw.
Mwingia, hata hivyo, ametoa rais kwamba mikakati ya kumkomboa mkulima
inayofanywa na Bodi hiyo isiishie kwenye nafaka pekee bali pia kwenye
sekta zingine muhimu kama vile ufugaji na uvuvi ambazo amesisitiza
zinahitaji msukumo huo ili kuimarisha tija.
Bi.
Petronella Mchechu wa Ngarenaro naye amesema hayo, akiongezea kwamba
amefarijika kuona CPB inafanya kazi na wakulima na watafiti mbalimbali
katika kudumisha ubora wa nafaka na mazao yalinayozalishwa nchini, na
kwamba wakulima wangekuwa mbali zaidi kimaendeleo endapo kama hatua hizo
zingekuwa zinachukuliwa toka zamani.
Post A Comment: