Na Heri Shaaban


MUFTI wa Tanzania Shekhe Abubakar Zuberi amewataka Watanzania kudumisha amani na mshikamano wasichafue hali ya hewa katika nchi yetu.

Shekhe Abubakari Zuberi aliyasema hayo Dar es Salaam leo katika Kongamano la dini ya Kiislam lililoandaliwa na Baraza Kuu la kiislam Tanzania BAKWATA kwa kushirikiana na Kituo cha Kiislam cha Misri .

Akizungumza katika kongamano hilo Mufti alisema tunajivunia amani iliyopo katika nchi yetu Tanzania hivyo tudumishe amani iliyopo kwa umoja wetu tusikubali hali ya hewa kuchafuliwa.


"Amani ndio jambo la msingi sana nawaomba Watanzania tudumishe umoja na mshikamano wetu tuzidi kuchapa kazi katika kuisaidia Serikali yetu na kuunga mkono Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu" alisema Mufti.


Mufti alisema amani iliyopo hapa nchini ni lulu tuendelee kudumisha mshikamano na kujenga uzalendo kwa ajili ya nchi yetu


Kwa upande wake Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum alisema Uislam kuchafuliwa sio vizuri kila moja anaitaji amani ,Wanyama na ndege pia wanaitaji amani wakikosa usalama unapomfuata ndege au Kunguru anaruka .


Shekhe Alhad alisema ,Waislam na Afrika wanaendelea kuombea amani katika nchi yetu na Afrika kwa ujumla huku wakijenga mausihano mazuri .

Aidha alisema katika nchi yetu kuna mausihano mazuri dini zote na wanaendelea kushirikiana pamoja wote marafiki baina ya dini hizo.


Mkurugenzi wa Kituo cha Kiislam Misri Tanzania Shekhe Jamal Abdulmdaty alisema Mafunzo hayo ya dini inatufunza uislam dini ya kweli na umoja tusaidiane katika wema na wale si waislam pia wasaidiane mtu atakaye muua mwezake awezi kuona pepo.
Share To:

Lucas Myovela

Post A Comment: