Kaimu Mkurugenzi Idara ya Makampuni na majina ya biashara ndugu, Meinrad T. Rweyemamu akiwasilisha taarifa ya namna ya usajili wa makampuni unavyofanywa na Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kwa Kamati ya kudumu ya bunge Viwanda, Biashara na Mazingira, iliyofanyika leo Juni 9,2021 Bungeni jijini Dodoma.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Ndugu Godfrey Nyaisa akitoa ufafanuzi wa baadhi ya masuala yaliyoulizwa na wabunge wa kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira katika kikao kilichofanyika leo Juni 9 2021 Bungeni jijini Dodoma.

Msajili msaidizi Mkuu miliki ubunifu kutoka BRELA Bi. Loy Mhando akitoa ufafanuzi katika kikao cha kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira katika kikao kilichofanyika leo Juni 9, 2021 Bungeni jijini Dodoma.

Kaimu Mkuu wa sehemu ya Leseni za Biashara akitoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja za waheshimiwa wabunge katika kikao cha kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira katika kikao kilichofanyika leo Juni 9,2021 Bungeni jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa kamati ya bunge Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. David Kihenzile (Mb) akizungumza wakati wa kikao cha kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira kupokea taaraifa ya utendaji wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) katika kikao kilichofanyika leo Juni 9, 2021 Bungeni jijini Dodoma.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) akitoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja zilizojadiliwa katika kikao cha kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira kupokea taaraifa ya utendaji wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kilichofanyika leo Juni 9, 2021 Bungeni jijini Dodoma.

Mbunge wa Jimbo la Bunda Vijijini Peter Mwita Getere, akichangia katika kikao cha kamati ya kudumu ya bunge Viwanda, Biashara na Mazingira kilichofanyika leo Juni 9, 2021 Bungeni jijini Dodoma.

Mbunge wa Jimbo la Buchosa Mhe.Eric Shigongo ,akichangia katika kikao cha kamati ya kudumu ya bunge Viwanda, Biashara na Mazingira kilichofanyika leo Juni 9, 2021 Bungeni jijini Dodoma.


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof Kitila Mkumbo amesema kuwa Serikali itaendelea kuiwezesha BRELA kuboresha utoaji wa huduma zake kwa wafanyabiashara kwa kuwa ni chombo muhimu katika ukuaji wa Sekta ya Biashara nchini.

Waziri Mkumbo ameyasema hayo wakati wa semina iliyolenga kuwaelimisha wajumbe wa Kamati hiyo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya BRELA na mafanikio yake iliyofanyika leo Juni 9,2021 katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.

Nayo, Kamati hiyo imeipongeza BRELA kwa kuboresha utendaji kazi na kuitaka iendelee kuongeza ubunifu katika kuboresha huduma na kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma hizo hadi vijijini.

Aidha, Wajumbe wa Kamati hiyo wametoa maoni na mapendekezo mbalimbali yanayolenga kuboresha huduma na bidhaa zinazotolewa na BRELA ikiwemo Uhuishaji wa taarifa, uhusiano wa biashara kati ya Tanzania Bara na Zanzibar, Umiliki Manufaa na Sera ya Taifa ya Umiliki Binafsi

Akiwaelimisha Wajumbe wa Kamati hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Bw. Godfrey Nyaisa alisema BRELA inaendelea kuboresha utoaji wa huduma zake kwa njia ya mtandao kwa kutumia mifumo mbalimbali ya Sajili kwa lengo la kuboresha mazingira ya biashara nchini.

Bw.Nyaisa pia amesema kuwa BRELA inaendelea kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mtaa na SIDO katika utoaji wa huduma, na imeingia makubaliano mbalimbali ya Kikanda na Kimataifa katika nyanja za umiliki wa ubunifu.

Amesema kuwa jukumu la msingi la BRELA ni kusimamia ufanyikaji wa Biashara nchini kwa kuzingatia sheria na kanuni za biashara zilizopo.

Afisa huyo amesema ili kuhakikisha kuwa mazingira ya uwekezaji, uanzishaji na urasimishaji biashara nchini yanakuwa wezeshi, BRELA imeandaa Mpango Mkakati wa saba unaoanza kutekelezwa mwaka 2021/22 na unalenga kuboresha utoaji wa huduma za sajili na leseni ili kuwa na ukuaji endelevu wa viwanda na maendeleo ya uchumi.

Hata hivyo amesema kuwa mpango huo umelenga kufanya maboresho ya sheria zinazosimamiwa na BRELA ili kuendana na mahitaji ya kibiashara ya sasa na mipango ya kitaifa.

Ametaja mambo yaliyotekelezwa hadi sasa katika mpango mkakati wa sita, Bwana Nyaisa alisema kuweka mifumo ya Kielektroniki ya Utoaji wa Huduma za Sajili (ORS) na Utoaji wa Leseni za Biashara (NBP).

Pia ametaja utengenezaji na uboreshaji wa mifumo ya utendaji kazi kama Mfumo wa ki-elektoniki wa Majalada – “e-Office”, Matumizi ya Mfumo wa Ulipaji Serikalini (MUSE), na Mfumo wa ki-elekroniki wa mahudhurio (e- Attendance System).

Bw.Nyaisa amesema pia uandaaji wa nyaraka mbalimbali za Kiutendaji na Kiutawala kama Mpango Mkakati – Strategic Plan 2021/22– 2025/26, Mkakati wa Mawasiliano na Huduma kwa Mteja (Communication and Customer Service Strategy), Kanuni za Utumishi, Fedha, na maendeleo ya Watumishi.

Share To:

Post A Comment: