Na Lucas Myovela _ Arusha.

Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe, Frank James Mwaisumbe, amewataka mawakala wa ujenzi wa barabara hapa nchini kushirikiana kwa pamoja katika kuboresha miundombinu ya haya ya barabara za wilaya zinazo onganisha mikoa hapa nchini.

Amesema hayo wakati wa ufunguzi wa Semina ya mawakala wa ujenzi wa barabara kutoka katika nchi saba za Africa, Mwaisumbe ambaye amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe John Mongela, katika mkutano huo amesema ni wakati wa Mawakala wa barabara katika mataifa yote kufanya kazi kwa pamoja ilikuondoa changamoto zinazo epukika.

Mwaisumbe ameeleza kuwa kumekuwa na changomoto kubwa katika ujenzi wa madaraja hasa katika Nchi za Afrika hasa mvua zinaponyesha hubeba ma daraja na kuacha ugumu kwa wananchi na kuweza kupunguza mapata kwa serikali hasa katika kuchochea ukuaji wa uchumi.

"Mawakala wote wa ujenzi wa  barabara mliyo hapa mnatakiwa kuwa wenye uharaka kwa wanachi ili kubora maiundombinu kwa jamii hasa katika ujenzi wa madaraja bora yenye kukizi mahitaji ilikuondoa changamoto zinazo epukika maana bado kunachangamoto ya barabara zinazo unganisha  barabara kubwa za miji". Ameeleza Dc Mwaisumbe.

"Kwa wakala wa hapa kwetu Tanroad kwa kushirikiana na Tarura wanatakiwa kuwa na takwimu husika ili kuondoa vikwazo vya barabara kwa wananchi wa vijijini maana huko ndiyo kuna mazao mengi yanayo leta mijini wanapaswa kuunganisha barabara za wilaya na mikoani tena ziwe barabara zente ubora kwa ukuaaji na ustawi wa uvmchumi kwa watanzania na taifa kwa ujumla". Ameeleza Dc Mwaisumbe.

"Kwa upande wa Nchi yetu tunajua serikali imefanya kazi kubwa kwa awamu ya tano na hii awamu ya sita inayo ongozwa na Mh Samia Suluhu Hassan, katika upande wa miundombinu hasa katika ujenzi wa barabara wamefanya kazi nzuri sana ingawa bado kuna changamoto kadhaa". Dc Mwaisumbe.

Kwa upande wake Katibu mtendaji wa chama cha barabara (TARA), Eng Hagai Bishanga ameeleza kuwa  ili kuwa na uchumi madhuti kunategemea sana miundombinu ya barabara kwa wanachi ambao ni wafanya biashara hasa katika nchi za Africa.

"Kwa mkutano huu mahususi wa  wataalamu wa barabara kutoka nchi hizi saba za Afrika tunategemea kuwa na mifumo endelevu za mifumo ya baraba baora kwa malengo ya kuchochea uchumi kwq mataifa yetu ambayo bado tunategemea miundombinu ya barabara kwa kiasi kikubwa". Eng Haghaid

"Ingawawa bado kunachangamoto mbalimbali hapa nchini ikiwemo fedha inayotengwa kwa ujenjenzi na matengenezo ya barabara bado haikidhi mahitaji, kutokujua takwimu za barabara na mifumo yake. Pia katila upande wa sera zetu za barabara bado kwasasa hazikidhi mahitaji inatakiwa sera zibadilishwe ili ziwe zenye kukidhi mahitaji ". Ameeleza Eng Haghaid

Inaelezwa kuwa lengo kuu la mkutano wa mawakala wa ujenzi wa barabara ni kujua na kupatiwa ufumbuzi wa changamoto za barabara katika nchi za Afrika ikiwemo Tanzania ili kuepusha serikali kuingia kwenge gharama kubwa katika ufanyaji wa matengenezo wa barabara.

"Ukubwa wa gharama za merekebisho ya barabara yanatokana na kutokujua takwizmu za sahihi za barabara zinahitaji nini, tunahitaji kuweka mifumo mizuri ya utambuzi wa uhitataji wa barabara ili kuisaidia serikali kutokufanya marekebisho makubwa ambayo gharama zake ni kubwa". Ameeleza mmoja wa washiriki.

Mkutano huo wa siku sita uliyoandaliwa na Tanzania Roads Association ( TARA ), lengo likiwa ni kutatua changamoto za miundo mbinu ya barabara katika ukanda wa Afrika, utakapo malizika unatarajiwa kuwa na manufaamakubwa katika utendaji katika nyanja ya miundombinu ya barabara katika ukuwaji wa maendeleo na uchumi katika ncho za Afrika.
Share To:

Post A Comment: