Na. Angela Msimbira Dar-Es Salaam


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  Mhe  Ummy Mwalimu  ameunda  tume huru  ya kuchunguza  kero na malalamiko  ya wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo na kutoa siku 14  kukamilika kwa uchunguzi huo


Ameunda tume hiyo  leo mara baada ya  kuongea na  wafanyabiashara wa Soko hilo katika ziara yake ya kukagua utendaji kazi na kusikiliza changamoto za wafanyabiashara wa Soko hilo , Jijini Dar-es-salaam


Waziri Ummy amesema kuwa baada ya kuwasikiliza wafanyabiashara hao amegundua kuwa lipo tatizo katika soko hilo ambapo amesema tatizo kubwa ni ukosefu wa mahusiano mazuri kati ya wafanyabiashara na  menejimenti ya  ya shirika la masoko la kariakoo,   uwepo wa tuhuma za rushwa kwa baadhi ya viongozi wa Soko, tozo za kubwa la kodi na  uwepo wa madalali wa  vigoli  pamoja na uwepo wa ubadhilifu wa fedha za mali za Shirika la Masoko  ya Kariakoo.


 Ameiagiza Tume hiyo kuhakikisha inapitia kwa kina malalamiko yaliyowasilishwa na wafanyabiashara hao ili yaeze kupatiwa ufumbuzi na Serikali kwa wakati na kufanyiwa uamuzi utakaosaidia kulipeleka taifa mbele katika kuhakikisha wafanyabaishara wanafanya biashara zao katika mazingira  mazuri kwa gharama zinazokubalika na Serikali


Akizungumzia uwepo wa madalali  Waziri Ummy  amesema kuwa kuna wapo madalali waliojimilikisha  vizimba na vigoli  katika soko hilo  ambapo wanawapingisha wafanyabiashara wadogo kwa gharama kubwa  hali hii inarudisha nyuma juhudi za Serikali za kuhakikisha watu wake wanapata maeneo ya kufanyia biashara ili kujikwamua kimaisha na kujiongezea kipato.


Aidha, ameiagiza Tume  huru ya uchunguzi  kuishauri Serikali kama upo umuhimu wa kuendelea kuwepo kwa Shirika la Masoko ya kariakoo kwa kipindi cha wakati wa sasa kulingana na mabadiliko ya kisayansi na Teknolojia.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: