Nyumba ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Singida iliyopo karibu na Msikiti wa Kati, Block H  No 13  ambayo ipo mbioni kupigwa mnada.

Mapokezi ya Kaimu Sheikh Nassoro baada ya kuwasili Shelui jana katika ziara yake ya kikazi ya siku moja. 

Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Singida Issa Nassoro (wa tano katikati) akiongoza kuomba dua mbele ya kaburi la Sheikh Yusuf Iddi Katalama ambaye alikuwa ni mmoja wa waanzilishi wa dini ya Kiislamu Bonde la Iramba wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja Shelui mkoani hapa jana. Wengine ni viongozi wa dini ya kiislamu wilayani Iramba.

Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Singida Issa Nassoro, akiongoza dua katika arobaini ya Marehemu Maalim Selemani Kingu.

Swala ikiendelea .

Sheikh wa Wilaya  ya Iramba,  Hussein Mgmbaika, akizungumza katika mkutano huo.

Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) Wilaya  ya Iramba, Ali Katembo, akizungumza katika mkutano huo.

Mwanafunzi, Ali Mohamed akisoma Qulaan katika mkutano huo.

Dufu likipigwa  katika mkutano huo.

Mzee Juma Kengele, akizungumza katika mkutano huo.

Mzee Abdallah Katembo, akizungumza katika mkutano huo.

Mzee Ismail Mang'oma, akizungumza katika mkutano huo.

Mjumbe wa Kamati ya Msikiti wa Kata ya Shelui, Ibrahim Kingu, akizungumza katika mkutano huo

Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Singida Issa Nassoro, akiingia Msikiti wa Kata ya Shelui kuzungumza na Waislamu.


Mkutano ukiendelea.

Dua katika arobaini ya Marehemu Maalim Selemani Kingu, ikiendelea. Kutoka kushoto ni Sheikh wa Msikiti wa Kata ya Shelui, Iddi Yusuf, Mjumbe wa Kamati ya Msikiti wa Kata ya Shelui, Ibrahim Kingu na Sheikh wa Msikiti wa Al-Jabir, Abdruazizi Ngololo ' Maarufu Sheikh Nyambo'


 Wakina Mama wakiwa katika Arobaini ya Marehemu Maalim Selemani Kingu.



Na Dotto Mwaibale, Singida 


KAIMU Sheikh wa Mkoa wa Singida Issa Nassoro amewaomba Waislamu mkoani hapa kuinusuru nyumba yao iliyopo mjini hapa isipigwe mnada.

Sheikh Nassoro alitoa ombi hilo  juzi wakati akizungumza na Waislamu wa Shelui katika ziara yake ya kikazi ya siku moja.

"Waislamu wenzangu nina ujumbe muhimu kwenu ambao nitawaachia Sheikh na Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) wilaya  ambao watausambaza hadi kwenye kata nao si mwingine tuna nyumba ya Bakwata ipo pale mjini karibu na Msikiti wa Kati ni Block H  No 13 inapigwa mnada.Kabla sijawa Kaimu Sheikh wa mkoa nilimfuata Mufti Sheikh Abubakar Zubery kumuomba kumuambia kwanini nyumba hiyo hiuzwe hivyo nilimuomba anipe jukumu la kusimamia suala hilo kwa maana ya kuepuka isipigwe mnada ndio maana nimekuja kwenu ili tuinusuru kwani zinahitajika Sh.Milioni 70 ambazo si pesa nyingi kwa watu wengi kwani tukifanya kila mmoja atoa Sh.10,000 kwa wilaya zote saba za Singida tutapata Sh.Milioni 47 na hizo zitakazo salia tutatafuta njia nyingine ya kuzipata ili tuigomboe nyumba hiyo tukijipanga  vizuri naamini hatutakosa fedha hizo" alisema Nassoro.

Katika hatua nyingine Sheikh Nassoro aliwataka Waislamu wa Mkoa wa Singida kuacha kugombana na kueleza kuwa kata, wilaya, mkoa na Taifa lenye magomvi haliwezi kupata maendeleo na ili maendeleo yapatikane kuanzia ngazi ya familia, jamii hadi katika nyumba za ibada nikuacha magomvi.

Aidha Sheikh Nassoro akizungumza na Waislamu hao alisema mbele yao wana majukumu mengi  makubwa na moja ya jukumu alilonalo ni kuboresha taaluma ya dini hasa katika shule mbalimbali za msingi na sekondari.

Alisema licha ya Serikali kuweka vipindi vya dini katika shule hizo kwa ajili ya kuwaelimisha vijana wa kiislamu kumekuwepo kusuasua na kuwa kwa mujibu wa Katiba ya Bakwata wenye jukumu la kusimamia vipindi hivyo ni baraza la masheikh wa kata waliopo kwenye maeneo zilipo shule hizo.

" Jambo ninalolisisitiza ni masheikh wa kata wajitahidi kutoa walimu katika kata zao ili vijana wa kiislamu waweze kupata taaluma za dini." alisema Nassoro.

Akizungumza katika mkutano huo Mzee Ismail Mang'oma alisema kazi kubwa ya kwanza ambayo Sheikh Nassoro anatakiwa kuifanya ni kuwaunganisha Waislamu wa Mkoa wa Singida na kuwa wamoja baada ya kupalaganyika kwa kila mtu kuwa kivyake.

Alitaja kazi ya pili ambayo anatakiwa kuifanya ni kuwainua waislamu kiuchumi.

Katika ziara hiyo Sheikh Nassoro alipata fursa ya kuzuru kaburi la Sheikh Yusuf Iddi Katalama ambaye alikuwa ni mmoja wa waanzilishi wa dini ya Kiislamu Bonde la Iramba pamoja na kuongoza dua katika arobaini ya Marehemu Maalim Selemani Kingu.

Share To:

Post A Comment: