Teddy Kilanga

Katika kupambana na haki sawa katika jamii Mkurugenzi wa Phide entertainment ,Phidesia Mwakitalema ameandaa tuzo kwa wanaume na vijana zikiwa na lengo la kuleta motisha kwa wanaume.


Akizungumza katika uzinduzi wa tuzo hizo jijini hapa ,Phide amesema kuwa tuzo hizo za wanaume zitatambulika Kama Extra Odinary Men Awards ,zikiwa ni Mara ya kwanza kufanyika ikiwa tuzo za wanawake zimeleta chachu ya maendeleo na kuhamasisha wajasiriamali wanawake kuboresha biashara zao zaidi.


"Ukiangalia tuzo za wanawake zilizofanyika mwezi wa tatu mwaka huu zililenga sehemu kuu tatu ikiwemo sifa ya kuwa mwanamke bora katika ujasiriamali,vikundi mbalimbali vya ujasiriamali ambao hufanya kazi pamoja pamoja na binti mjasiriamali,"amesema Mkurugenzi huyo.



Nae Katibu wa siasa na uwenezi jiji la Arusha ambaye pia Ni mgeni Rasmi wa hafla hiyo, Gerald Munisi amesema kuwa tuzo hizo zitakuwa chachu kwa viongozi wote kwani walishazoea kupatiwa wakati wa Mei Mosi tu,hivyo kupitia tuzo hizo zitawaongezea motisha ili kufanya kazi zao kwa weledi.


Elizabeth Mayani Ni mshindi wa tuzo za mwanamke tuzo ambapo ameibuka kidedea kupitia nafasi ya mwanamke mjasiliamali katika kampuni ya Newlook Briadle na kubaisha kuwa kupitia tuzo hizo imemsaidia kujulikana na kutangaza biashara yake kwa watu wengi



Aidha mwanamuziki wa Chama Cha wanamuziki Tanzania (Tamufo) Frank Richard Amesema kuwa tuzo za wanaume Ni tuzo nzuri ambazo zitawaonyesha wanaume ambao hawajulikani na kuwafanya kuwa mstari wa mbele katika jamii.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: