Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora (TBS) Bw.Mosses Mbambe (katikati) akifuatiliakikao kazi na Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFFA) kilichofanyika leo katika ofisi za Makao makuu TBS leo Jijini Dar es Salaam.

Mawakala wa wa Forodha (TAFFA) wakifuatilia kikao kazi ambacho kiliwakutanisha na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kujadili ni namna gani wanaweza kutatua changamoto zao katika utendaji kazi wao.


NA EMMANUEL MBATILO

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wamekutana na wanachama wa chama cha Mawakala wa Forodha (TAFFA) kwaajili ya kujadili ni namna gani wanaweza kuboresha utendaji kazi wao katika kuhakikisha wanakuza biashara na kumlinda mtumiaji.

lengo ni kuwapitisha katika taratibu za ukaguzi na upimaji wa bidhaa ambao unafanya na shirika hilo na vilevile wamewapitisha katika mfumo wa electronic window system ili waufahamu namna ya kuutumia na kurahisisha utoaji wa mizigo katika vituo vya forodha.

Akizungumza mara baada ya mkutano huo Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora (TBS) Bw.Mosses Mbambe amesema kuwa changamoto iliyopo kwasasa ni utumiaji wa mfumo wa electronic window system inaonekana kwamba baadhi ya mawakala hawaufahamu mfumo huo na kuweza kupelekea ucheleweshaji wa utoaji wa mizigo kutoka katika vituo vya forodha.

"Kama hauwezi kutumia huu mfumo kuna athari zinaweza kujitokeza hasa kuchelewesha mzigo kutoka katika kituo cha forodha na mzigo ukichelewa kutoka ina maana mteja hataweza kupata mzigo wake kwa wakati vilevile inaweza kupelekea mlundikano wa mizigo katika vituo vya forodha". Amesema Bw.Mbambe.

Kwa upande wake Meneja wa masuala ya ukaguzi wa bidhaa zinazotoka nje (TBS) Mhandisi Saidi Mkwawa amesema kuwa kuna baadhi ya mawakala wamekuwa wakilalamika kuna tatizo kwenye mfumo wa kuweza kufanya usajili na kuweza kutoa nyaraka zao kwaajili ya kufanyiwa ukaguzi ambapo kumekuwa na changamoto mbalimbali.

"Dhamira ya Serikali ni kumuepushia usumbufu yule wakala ambaye anafanya biashara kwasababu mfumo huu zamani kila unaemuona wakala wa forodha alikuwa lazima aweze kufanya maombi ya mifumo mbalimbali, aende Shirika la wakala wa meli TASAC, afike TBS kwenye mfumo tofauti ama aende kwenye mifumo mingine ya serikali. Lakini serikali ikaona yakwamba kuwe na mfumo mmoja ambao utarahisisha na kutoa ufanisi lakini kila jambo jipya linalokuja lazima liwe na changamoto zake". Amesema Mhandisi Mkwawa.

Nae Katibu Mtendaji (TAFFA) Bw.Elitunu Mallamia amesema kuwa kupitia mkutano huo unazidi kukuza mahusiano yao na TBS ambao wanashirikiana nao kwenye kusaidia nchi iweze kuingiza bidhaa bora na bidhaa ambazo zitawalinda watumiaji.

Sambamba na hayo Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Masoko (TBS), Bi.Gladness Kaseka amewakaribisha wadau mbalimbali wanaoona kuna changamoto wanazipitia katika utendaji ili waweze kufanya nao kikao na kujadili ni namna gani wanaweza kumaliza ama kupungua changamoto hizo.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: