Diwani wa Kata ya Mkinga Salehe Mtindi kulia akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa Michuano ya Fufua Cup Nahodha wa timu ya Kichalikani Ally Zairina baada ya timu hiyo kuifunga timu ya Moa Original bao 1-0 kwenye mchezo wa Fainali uliochezwa uwanja wa Kastamu

Diwani wa Kata ya Mkinga Salehe Mtindi kulia akimkabidhi Jezi Seti moja,mpira na firimbi wa Nahodha wa timu ya Moa Originali baada ya timu hiyo kuibuka mshindi wa pili kwenye  Michuano ya Fufua Cup kwenye mchezo wa Fainali uliochezwa uwanja wa Kastamu
Diwani wa Kata ya Mkinga Salehe Mtindi akizungumza wakati wa fainali ya mashindano hayo ambapo alimshukuru Muandaaji wa Mashindano ya Fufua Cup Jumaa Mohamed na kudhaminiwa na Saidi Duvii yalikuwa na lengo la kusaidia,kuendeleza na kukuza vipaji vya wachezaji chipukizi wenye vipaji vya mchezo wa mpira wa miguu wanaoishi wilayani Mkinga  na huchezwa kila mwaka
Muandaaji wa Mashindano ya Fufua Cup Jumaa Mohamed na kudhaminiwa na Saidi Duvii akiangalia vipaji vya wachezaji wachanga ambao wamechaguliwa kwenye mashindanio hayo

NA MWANDISHI WETU, MKINGA

TIMU ya soka Kichalikani FC ya wilayani Mkinga imetawazwa kuwa Mabingwa wapya wa Michuano ya Fufua Cup baada ya kuibamiza Moa Originali bao 1-0 katika mchezo wa Fainali uliochezwa kwenye uwanja wa Kastamu uliopo Kata ya Moa wilayani humo.

Kutokana na kuchukua Ubingwa hao Kichalikani FC waliweza kukabidhiwa Kombe ,Jezi 16,mpira 1,virimbi 1 huku mshindi wa pili Moa Originali akipata Jezi 16 ,Firimbi 1,mpira 1 wakati mshindi wa tatu ambao ni vibambani FC wakizawadiwa mpira 1,firimbi 1 na soksi 16,

Mashindano hayo ambayo yaliandaliwa na Jumaa Mohamed na kudhaminiwa na Saidi Duvii yalikuwa na lengo la kusaidia,kuendeleza na kukuza vipaji vya wachezaji chipukizi wenye vipaji vya mchezo wa mpira wa miguu wanaoishi wilayani Mkinga  na huchezwa kila mwaka.

Katika mchezo huo wa fainali ambao ulikuwa na upinzani wa hali ya juu uliwachukua dakika 60 timu ya Kichalikani kuweza kuandika bao lao la ushindi kupitia Amiri Ally ambaye alitumia uzembe wa mabeki wa wapinzani wao kupachika wavuni mpira huo.

Baada ya kuingia kwa bao hilo Moa Originali walirudi kujipanga na kuanza kupeleka mashambulizi mfululizo langoni mwa wapinzani wao bila mafanikio kutokana na kwamba kila mashuti yaliyokuwa yakielekezwa langoni mwao yalikuwa yakitoka nje ya lango.

Alisema Mashindano hayo yalishirikisha timu 16 zilizopo kwenye Kata 12 kutoka Tarafa ya Mkinga  lengo lao ni kutaka klabu hiyo kupenda wilaya nzima ili kuvutia wananchi kupenda vya kwao.

Aidha alisema kwamba lengo kubwa la  Fufua Cup ni kutaka kurudisha hamasa ya michezo wilayani Mkinga  huku akieleza ligi hiyo ilikuwa ichezwa wilayani nzima katika kata 22 ili kuleta thamani kwa kikosi ambacho kitaundwa kuanzia ngazi ya kitongoji ,kijiji hadi Kata.

Hata hivyo alisema kata ambazo hazikishiriki kwenye mashindano hayo zitafikiwa kwa mfumo wa mashindano ya ligi ya wilaya ambayo yameanza Aprili 10 mwaka 2021 ili wachezaji watakaochaguliwa wawezsha kuungana na wenzao kuunda kikosi cha timu ya Mkinga FC

“Lakini labda niseme tu kwamba Fufua Cup ni mradi ulioanzishwa kwa ajili ya kuwasaidia, kuendeleza na kukuza vijana wenye vipaji vya michezo vya mpira wa miguu wanaoishi katika Halmashauri ya Mkinga walio shindwa kuendeleza vipaji vyao na kukosa fursa za kujiunga na timu kubwa kutokana na mazingira wanayoishi”Alisema

Alisema kwamba mazingira ambayo wamekuwa wakiishi ambayo hayana wadhamini wa kukuza na kuendeleza vipaji hivyo na kupelekea kuua au kupoteza vipaji vyao na mwisho kuijingiza katika wimbi la kuwa wazazi au kuingia kwenye ndoa  za utotoni, kuingia kwenye matumizi ya madawa ya kulevya, Kupata Virusi vya HIV/AIDS.

“Hata wengine kuingia kwenye udokozi wa mali za watu  kwasababu yakukosa mbadala au suluhisho litakalo wawezesha kujikwamua au kukuza vipaji vyao ilikuwakuzia uchumi wao”Alisema

Alisema mradi huu utakuza Vipaji vya michezo, Afya, Ajira kwa Vijana na kukuza uchumi  kuanzia ngazi za Familia, Kijamii, na Kitaifa kwa Maendeleo Endelevu.

Mratibu huyo alisema madhumuni ya Ligi hiyo ni kutafuta wachezaji watakao wakilisha timu ya wilaya itakayoitwa MKINGA FOOTBALL CLUB ili baadae kuja kucheza Timu za Taifa na Kimataifa.

Hata hivyo alisema pia wana malengo ya shule yao na uwanja wa mazoezi wao wenywe na vifaa vya michezo kwa ajili ya kusimamia,kukuza na kuendeleza vipaji chipukuzi vya wachezaji wilayani humo.

Mwisho.

 

 

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: