Taasisi ya Wezesha Foundation inayojihusisha na masuala ya uwezeshaji vijana na Wanawake imefungua kituo maalumu  cha kuongeza ujuzi (Skills hub )  mkoani Kigoma. Kituo hicho kitajihusisha  na utoaji wa mafunzo mbali mbali   ya kuwajengea uwezo vijana na wanawake  katika uongozi na shughuli mbali mbali za kiuchumi.


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kituo hicho, Katibu Mtendaji wa taasisi hiyo Mhe. Zainab Katimba (Mb.) amesema mbali na kutoa mafunzo hayo kituo hicho kitakuwa kikitoa taarifa za fursa mbalimbali  za Vijana na Wanawake katika  mkoa wa Kigoma ikiwa ni pamoja na kusaidia walengwa kunufaika na fursa hizo. 


Aidha taasisi hiyo imetoa mashine 14 za kukoboa na kusaga nafaka kwa vikundi saba vya mfano katika halmashauri  saba mkoani Kigoma. Lengo kuu likiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano  ya kujenga uchumi wa viwanda na kuwawezesha vijana na Wanawake kiuchumi.


Taasisi hiyo ambayo imeanzishwa mwaka 2017 tayari imefanya shughuli mbalimbali mkoani humo ikiwemo kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana na wanawake zaidi ya elfu moja, mafunzo ya uongozi kwa madiwani wanawake, kutoa misaada katika sekta ya elimu na afya.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: