Monday, 1 February 2021

WAIPONGEZA SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA RAFIKI UANZISHWAJI VIWANDA

Na Ahmed Mahmoud Babati Baadhi ya wafanyabiashara Mkoani Manyara wameipongeza serikali kwa kuondoa urasimu katika uwekezaji wa viwanda ,Jambo lililowahamasisha kuanza ujenzi wa viwanda mbalimbali vya uzalishaji. Mmoja ya wafanyabiashara hao ,David Mulokozi ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa kiwanda Cha kutengeneza vinywaji vikali Cha Mati Super Brands LTD kilichopo mjini Babati ,ameliambia gazeti hili kwamba Sera ya Rais John Magufuli ya Tanzania ya Viwanda imemfungua macho na kuamua kuanzisha Viwanda vya uzalishaji. "Nilifanikiwa kufungua kiwanda kimoja Cha pombe kali Mwaka 2017 lakini hadi Sasa nifungua mefika viwanda vingine vitatu vya pombe Kali na pia nipo mbioni kufungua kiwanda kingine Cha dawa za binadamu baada ya serikali kuwatengenezea mazingira mazuri ya uwekezaji"amesema. Amesema kuwa baada ya rais Magufuli kuingia madarakani Mwaka 2015 na kuja na sera ya ujenzi wa viwanda,Jambo hilo lilimhamasisha na kuamua kuanzisha kiwanda wilayani humo ambacho kimekua na kuzalisha viwanda vingine viwili na Sasa yupo mbioni kuanzisha kingine Cha dawa za binadamu Amesema viwanda hivyo vinazalisha vinywaji vikali aina ya Sed Pineapple Flavored Gin, Strong Dry Gin , Strong Coffee Flavored Gin New to be Launched na Tanzanite Premium Vodca. Amesema kuwa tangu ameanzisha kiwanda hicho Mwaka 2017 amezalisha ajira zaidi ya 150 huku akitoa kipaumbele kwa wananchi wanaoishi jirani na kiwanda chake ikiwemo kuwajengea Mundo mbonu. "Niliamua kuanzisha kiwanda nikiwa na mtaji wa shilingi milioni 20 hasa baada ya kuvutiwa na sea ya Rais Magufuli ya ujenzi wa viwanda ,Sasa hivi mtaji wangu umekuwa na wala sitegemei mkopo kutoka sekta za fedha "Alisema Mulokozi. Amefafanua kwamba kabla ya kuanzisha kiwanda hicho alikuwa ameajiriwa kwenye kiwanda Cha mtu jijini Arusha kama afisa masoko lakini baada ya rais Magufuli kuanza kuhamasisha watu kujenga viwanda ,aliamua kuacha kazi na kufungua kiwanda chake mjini Babati. "Tuimefungua vituo vya mauzo katika mikoa mbalimbali hapa nchini ikiwemo,Arusha, Kilimanjaro ,Tanga, Dar es Salaam, Morogoro,Mwanza na Mikoa mbalimbali hapa nchini na nchi jirani ya DRC Kongo,Kenya ,Rwanda,Zambia, Malawi, na Burundi"Amesema Ameongeza kuwa matarajio yake ni kuwa na kiwanda kikubwa kinachoongoza kwa mauzo hapa nchini na ulipaji mzuri wa Kodi ya serikali. Amesema Siri ya mafanikio ni usimamizi na ufuatiliaji pia kuajiri wataalamu wenye ujuzi ,kujua masoko na kuepuka kutegemea mikopo mikubwa katika kuendesha biashara yako. Amewashauri wafanyabiashara wengine kutumia fursa hii ya raisi Magufuli kuanzisha viwanda na kutoogopa TRA kwani urasimu uliokuwapo hapo awali kwa Sasa umekwisha.

No comments:

Post a Comment