Monday, 1 February 2021

MAHAKAMA ITAFAKARI MIAKA 100 ILIYOPITA NA KUFANYA UTAFITI WA MIAKA MINGINE 100.
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.


Askofu KKKT Dayosisi ya Kaskazini kati  Askofu Dkt Solomon Massangwa ameitaka mahakama kuu kanda ya Arusha kutafakari miaka 100 iliyopita na kufanya utafuti wa miaka 100 mingine ijayo.


Askofu Dkt Masangwa alitoa rai hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria yaliyoenda dambasha na  maadhisho ya miaka 100 ya  tangu kuanzishwa kwa mahaka kuu hapa nchini  ambapo alisema kuwa ni vema watendaji wa mahaka wakatafakari walichokifanya miaka 100 iliyopita ili kuboresha miaka 100 mingine wanayoianza.Alieleza ni vyema baada ya kupata majibu ya walichokifanya, wakafanya utafiti wa namna watakavyoenda katika miaka mingine ili kuboresha upatikanaji wa haki na sheria katika nchi ya Tanzania. 


Aidha aliiombea na viongozi wake, mahakama na watendaji wake ili wa wewe kutekeleza wajibu wao kwa kuangalia sheri na kuzitafakari ili taifa liweze kustawi na kufanikiwa.


"Ninaomba kwaajili ya bunge ambao ndi wanahusika katika kutengeneza sheria lakini pia kwaajili ya mahakama ambao ndio wanahusika kutafsiri sheria ili wazikatie kufanikiwa kwa nchi yetu na kustawi kwa taifa letu,"Alisema Askofu Dkt Massangwa. Jaji mfawidhi wa mahakama hiyo Mosses Mzuna alisema kuwa  Jamuhuri ya muungano wa Tanzania awali ikiitwa Tanganyika ilikuwa ni koloni la Mwingereza baada ya Ujerumani kushindwa katika vita ambapo ilipelekea  kuanzishwa kwa sheria za Uingereza na mfumo wao wa mahaka kuu.


Alieleza hadi nchi kupata uhuru 1961, zilianzishwa mahakama za chini na maamuzi ya mahakama kuu yalihusu kesi za madai na jinai ambapo majaji waliteuliwa lakini ajira zao zilikoma kadri itakavyompendeza mfalme wa Uingereza.


Alifafanua kuwa  mada ya maadhimisho hayo imejikita katika utangulizi wa katiba ya nchi ambapo wao kama wananchi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania wameamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yao jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, udugu na amani.


"Misingi hii inaweza kutekelezwa tuu katika jamii yenye demokrasia ambayo serikali yake husimamiwa na Bunge lenye wajumbe waliochaguliwa na wanao wawakilisha wananchi na yenye mahakama huru zitakazo tekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote na kuhakikisha haki zote za binadamu zinadumishwa na kulindwa na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu"Alisema Jaji Mzuna.


kwa upande wake Veritas Mlay wakili wa serikali wa mkoa aliwasihi wadau wote wa sekta ya sheria kufikiria kutoka kwenye adhabu za gerezani na kuinhia katika adhabu za nje ili kuepusha misongamano ya wafungwa katika magereza.


"Adhabu za nje zitasaidia kuondoa msongamano itachangia watu kubadilika kwani jamii itawaona wazi wakiwa wanatumikia adhabu hizo,"Alisema wakili Veritas Mlay.


Naye mwenyekiti wa chama cha mawakili wa kujitegemea Tanganyika (TLS)  kanda ya Arusha Elibariki Maeda alisema kuwa bado kuna visingizio vya ucheleshaji wa kesi kwa kisingizio cha kutokukamilika kwa upelelezi jambo ambalo linachelewesha utoaji wa haki.


"kutokana na hili tunaiomba mahaka kurekebisha au kubadisha sheria ya utoaji wa dhamana kwa watuhumiwa hata kama upelelezi haujakamilika na pia naiomba serikali kuongeza idadi ya majaji ili kuweza kukidhi mahitaji ya wananchi wanao fika kupata huduma katika mahakama zote hapa nchini," Alisema maeda.

No comments:

Post a Comment