Nteghenjwa Hosseah, Mbeya


Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Dr. Ntuli Kapologwe amehuzunishwa na utendaji kazi wa Kamati ya Uendeshaji wa huduma za Afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunja(CHMT), Mkoani Mbeya unaopelekea kuzorota kwa huduma za Afya Wilayani humo.


Dr. Ntuli ameonyesha hali hiyo wakati wa ziara ya usimamizi shirikishi kwenye Mikoa na Nyanda za juu kusini ambapo alitembelea Halmashauri ya Chunya mapema Tarehe 15/02/2021.


Akiwa Wilayani humo Dr.Ntuli alikutana na CHMT na kutembelea Hospitali ya Wilaya ya Chunya pamoja na Zahanati ya Makongorosi.


Wakati wa kikao na CHMT, Dr. Ntuli alibaini kukosekana kwa ushirikiano baina ya wajumbe wa Timu hiyo na kupelekea kukosekana kwa uratibu thabiti wa shughuli zote za Afya Wilayani humo.


“Kuanzia kwenye uwasilishaji wa taarifa mnaonekana kabisa hamko pamoja taarifa hamjaimiliki na bado inaonyesha mapungufu  katika utoaji wa huduma za Afya mnazozisimamia” Alisema Dr Ntuli.


CHMT ambayo haiko pamoja haiwezi kusimamia vizuri utoaji wa huduma za Afya kama mnashindwa kujisimamia kama Timu mnadhani mtaweza kusimamia vituo vilivyo chini yenu? Alihoji Dr Ntuli.


Alipotembelea Hospitali ya Wilaya ya Chunya alibaini usimamizi duni wa mapato ya Serikali, ungalizi hafifu wa Uhifadhi wa chanjo pamoja na utoaji na ukaguzi wa dawa.


“ Hospitali hii sio ya kukusanya chini ya laki tano kwa siku inaoenekana kuna mahali mapato yanavuja idadi ya watu wanaokuja kutibiwa hapa ni kubwa sasa kwanini hakuna mapato.


Ukiangalia menejimenti ya chanjo haiko vizuri na wakati hili ni eneo nyeti sana kwa ajili ya Afya za watoto wetu kwanini nyie mnachukulia kawaida, chanjo inatakiwa kuhifadhiwa kwenye ubaridi ulioelekezwa hapa naona kuna vitu hamvizingatii katika uhifadhi wa chanjo” 


Zaidi ya hapo alipotembelea Zahanati ya Makongorosi alikutana na idadi kubwa ya wagonjwa wanaosubiria kupata huduma katika Zahanati hiyo ambayo katika taarifa walionyesha kukusanya shilingi elfu kumi kwa siku huku mganga mfawidhi akieleza kuwa wagonjwa wengi wanaotibiwa hapo ni wale wa msamaha.


Pamoja na hayo Dr. Ntuli hakuridhishwa na hali halisi ya usafi wa kituo pamoja na huduma zinazotolewa.


“Haiwezekani wananchi wote hawa wanapata huduma katika mazingira machafu namna hii hapa ni hospitali lazima tuonyeshe mfano timu za Afya zinafanya kazi gani kwanini vitu vya kawaida kama hivi ambavyo vingine havihitaji hata fedha havifanyiki.


Niwatake CHMT pamoja na wataalamu wa Zahanati ya Makongorosi kufanya usafi wa kina katika Zahanati hiyo na kuondoa vitu vyote visivyotumika ili kupunguza mlundikano” alisema Dr Ntuli.


Pia aliwaagiza CHMT kufanyia kazi maelekezo yote aliyotoa na kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kama Timu na kuongeza usimamizi katika vituo vya kutolea huduma ili kuboresha utoaji wa huduma za Afya.


Mwisho.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: