Naibu Waziri wa TAMISEMI David Silinde amewasimamisha kazi wakuu wa shule wawili wa sekondari za Bahati Day na Muktuka kwa kushindwa kusimamia ujenzi wa mabweni ya shule hizo kwa kutumia gharama kubwa huku ujenzi ukiwa bado haujakamilika tofauti na muongozo ulitoka ofisi ya TAMISEMI uliotaka kwa milion 80 bweni liwe limekamilika.


Naibu waziri Silinde amesema katika halmashauri ya Babati vijijini amejionea ujenzi wa mabweni mawili ambayo hatua nzuri kukamilika wakiwa wamejenga  mabweni mawili kwa milion 74 tu kati ya Mil 160 walizopatiwa na serikali tofauti na Babati Mjini ambapo kwa kila shule ya sekondari moja imetumia zaid ya mil 80 katika hatua ya upauzi. Huku taarifa za gharama za Shule hizo mbili zikiwa zimefanana kwa kila kitu.


Silinde ameagiza uchunguzi wa kina kujua fedha hizo zimetumikaje katika shule hizo mbili za halmashauri ya babati mjini na hatua kali za kisheria kuchukuliwa kwa watu wote waliohusika katika matumizi mabaya ya fedha na kuvunja kamati zote za ujenzi katika shule hizo mbili za babati mjini na kuagiza ziundwe kamati za ujenzi upya na kuteuliwa kwa makaimu wakuu wa shule watakao simamia ujenzi huo mpaka kukamilika wakati uchunguzi ukiendelea.


Aidha Naibu waziri Silinde ameagiza Afisa elimu wa Sekondari wa Babati mjini kuandika barua kwenda ofisi ya TAMISEMI ya kwanini asichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kushindwa kusimamia miradi hiyo huku mhandisi wa Halmashauri ya Babati Mjini naye akikutana na lungu hilo la kuandika barua ya kujieleza kwanini ametoa ushahuri ambao si sahihi wa matumizi  ya bei ya juu ya ujenzi tofauti na maelekezo ya serikali.


Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange amesema kwasasa ameunda kamati ya uchunguzi kutoka TAKUKURU kutokana na kutoridhika na gharama za ujenzi wa mabweni hayo mawili kuwa kubwa tofauti na gharama waliyotumia wenzao wa Babati vijijini ambao wametumia gharama ndogo na ujenzi ukiwa unakaribia kuisha.

Share To:

Post A Comment: