Saturday, 2 January 2021

NAIBU MEYA ILALA AELEZA MIKAKATI YA UTEKELEZAJI WA ILANINA HERI SHAABAN


NAIBU MEYA wa halmashauri ya ILALA Saady Kimji  aeleza mikakati ya utekeleza wa Ilani 2025.Naibu Saady Kimji alielezea utekekeza wa Ilani Leo katika chakula cha mchana wakati wa kuwashukuru wajumbe wapiga kura wake wa kata ya Ilala. Kimji alisema katika utekelezaji wa Ilani mikakati yake kujenga soko  la kisasa  Ilala  na Kituo cha Afya ambapo kata hiyo itakuwa ya kisasa  kwa kuboresha huduma za afya.


" Mikakati yangu  tunatafuta  eneo kwa ajili ya kujenga kituo cha afya fedha ipo tayari shilingi milioni 200 pia tunajenga soko kubwa la Ilala Boma kutokana na soko lililopo dogo watu wafanyabiashara wengi '"alisema Kimji


Mikakati mingine katika sekta ya elimu kuongeza shule waweze kuwa na kidato cha tano na kidato cha sita awali kata ya Ilala ilikuwa aina Shule ya sekondari Juhudi kubwa amefanikisha Mbunge wa Ilala Mussa Zungu na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri katika sekta ya elimu Wanafunzi wanafanya vizuri kitaaluma.


Akielezea ushindi wa Chama cha Mapinduzi CCM aliwapongeza kwa kufanikisha Ushindi kwa asilimia 78 amewataka wajumbe kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo  wanapoandaa mikutano Wenyeviti Washirikishe Chama cha Mapinduzi  CCM


Aidha pia aliwataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Watendaji kutatua kero ngazi ya mtaa kuisaidia Serikali kwani ni sehemu ya majukumu yao ya kazi wasiyakwepe. Aliwataka Wenyeviti wa Serikali za Mtaa na Watendaji wawe wadilifu 

wafanye kazi kwa bidii  waunge mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli katika kujenga TANZANIA ya Uchumi wa viwanda


Kwa upande wake Mratibu wa Polisi Jamii Kariakoo  Inspector Mayamba Adam aliwataka wajumbe wa mashina na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa washirikiane kutoa taarifa za waamihaji haramu endapo wataficha  kutoa   watawashugulikia. Kamanda.


Ispector Adamu aliwata washirikiane katika masuala ya Ulinzi na Usalama katika Kata hiyo 

Mwisho

No comments:

Post a Comment