Na Ahmed Mahmoud Mererani Chama Cha wachimbaji wa Madini ya Tanzanite Mkoa wa Manyara (MAREMA)kimewatahadhalisha wachimbaji wadogo wa Madini hayo(Wanaapolo)wanaojihusisha na utoroshaji wa Madini kuacha mara moja kwani kwa kufanya hivyo watakabiliwa na adhabu ya kufungiwa kuingia mgodi wowote wa madini nchini kwa miaka kumi. Aidha aliwataka wachimbaji hao kuhakikisha wanapatiwa mikataba inayoeleweka na kitambulisho kutoka kwa wajiri wao jambo litakalosaidia wao kudai haki zao kwa wamiliki wa migodi na kuacha kutorosha Madini kwa kisingizio Cha kutolipwa mshahara. Kauli hiyo imetolewa Jana na katibu wa Marema tawi la Mererani, Recho Njau wakati akiongea na mamia ya wanaapolo katika machimbo ya Madini yaTanzanite , Mererani nwilayani Simanjiro,mkoanwa Manyara na kuwataka kuwa wazalendo na nchi yao na kutokukubali kurubuniwa na wachuuzi wa Madini hayo. "Mwanaapolo yoyote atakayekamatwa na jiwe akitorosha hataruhusiwa kuingia kwenye mgodi wowote wa Madini hapa nchini kwa miaka 10 na adhabu ya kifungo jela na picha yake itasambazwa katika migodi yote nchini"alisema Recho. Hata hivyo aliruhusu wachimbaji hao kuuza Madini yao ndani ya mgodi huo kwa wenye leseni na kuepuka kuyaficha kwa nia ya kutorosha nje ya ukuta. Awali hoja ya Katibu huyo ya kutaka wachimbaji hao wapekuliwe punde wanapotoka shimoni ilizua tafrani katika kikao hicho walidai Jambo Hilo haliwezekani kwani Baadhi ya wamiliki wa migodi hawawalipi. Naye Mwenyekiti wa wanaapolo Iddy Kondo alisema wachimbaji wapo tayari kufuata maelekezo yoyote ya serikalini ikiwemo kuacha kutorosha Madini ila wameomba serikali kuweka mazingira mazuri ya wao kunufaika na rasilimali hiyo kwa kuwa ndio wazalishaji wakuu lakini wamekuwa hawalipwi na wamiliki wa migodi. "Tunaiomba serikali iwaoatie fursa wanaapolo kuwez kuuza mawe yake pindi anapotoka migodini kwani wachimbaji wengi hawajaajiriwa nanhiyo itakuwa sulujisho la kutorosha mawe"alisema Kondo. Katika hatua nyingine,fundi sanifu mkuu kutoka tume ya Madini Mererani ,Antony Kusaga akisisitiza kuwa lazima wanaapolo wapekuliwe pindi wanapotoroka mgodini kauli ambayo ilizua tafrani kwa wachimbaji hao na kusababisha Baadhi yao kutawanyika. "Mwanaapolo ambaye atatoka mgodini lazima ajisalimishe kwa meneja wa Mgodi kuwa anajiwe ili likafanyiwe tathimini "alisema Kusaga.
Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: