Saturday, 9 January 2021

DR. TULIA AWAOKOA WANAFUNZI WA SEKONDARI MBEYA KWENYE TABU YA MADARASA

 


Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini ambaye pia ni Naibu Spika Dr. Tulia Ackson amefanya ziara katika Shule za Sekondari Sinde na Wigamba zilizopo wilayani hapo kwa lengo la kujionea ujenzi na ukarabati  wa madarasa unaoendelea katika shule hizo zilizopo maeneo tofauti ambapo pia ametoa msaada wa mifuko 100 ya Cement katika kila shule ili kusaidia ujenzi huo kukamilika haraka.


Akizungumza na Wazazi pamoja na Wanafunzi kwa nyakati tofauti waliojitokeza kumsikiliza, Dr. Tulia akiwa Sinde amesema >>>”Kwanza niwashukuru sana Wananchi kwa ushirikiano mkubwa sana mnaouonesha kwa Serikali yetu, madarasa haya tunayoyaona ni wazi kama wazazi mmejitoa sana na kwa niaba ya Serikali tunawashukuru sana kwa huu uzalendo wenu wa kujitoa ikiwemo kuchangishana fedha kidogokidogo kwa ajili ya ujenzi huu”


“Leo tumekuja kutoa mchango wa mifuko 100 ya Cement ili iweze kusaidia kumalizia ujenzi huu wa madarasa ambao unaendelea hapa katika shule ya Sekondari Sinde ikiwa ni muendelezo wa ushirikiano wetu ambao tulishauanza tangu huko mwanzo na ningetamani ushirikiano wetu huu uendelee kwa ajili ya kuwasaidia hawa watoto wetu wapate elimu katika mazingira yaliyo bora kabisa”- Dr. Tulia Ackson


“Sasa baada ya kuwashukuru wazazi naomba niseme kidogo na wanafunzi, nyinyi watoto wangu niwaombe sana sana mjitume katika masomo yenu ikiwemo kutanguliza mbele bidii na nidhamu ili muweze kuzifikia ndoto zenu. Sisi wazazi wenu tunatamani sana tunapowawekea mazimgira bora ya kusoma basi na nyinyi mtuletee matunda bora ya ufaulu kwenye masomo yenu”-Dr. Tulia Ackson


Akiwa katika Shule ya Sekondari Wigamba, Dr. Tulia pia amesema>>>”Kama nilivyozitoa pongezi katika shule ya Sinde, nitoe pongezi pia kwenu wazazi wa hapa Wigamba kwa namna mnavyojitoa katika shughuli hizi za maendeeo. Wapo wanaosema hizi ni kazi za Serikali, Serikali itafanya yake na sisi wananchi tunajukumu la kuungana kutekeleza majukumu yetu”


“Asiwepo mtu wa kuturudisha nyuma hivyo basi tuendelee kushikamana katika shughuli za maendeleo kama hizi kwa ajili ya faida zetu na watoto wetu na katika kuweka msisitizo kwenye hilo, baada ya kuona umoja wenu mliouonesha katika ujenzi wa madarasa hapa shuleni basi na mimi leo nimekuja na mifuko 100 ya Cement kwa ajili ya kuongeza nguvu ili kusaidia kuhakikisha ujenzi huu unakamilika ndani ya wakati”-Dr. Tulia Also

No comments:

Post a comment