Waziri wa Madini Doto Biteko akizungumza wilayani Chunya leo kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila akizungumza kulia ni  Waziri wa Madini Doto Biteko


Na, Tito Mselem, Chunya

Waziri wa Madini Doto Biteko, amefuta Leseni Sita za Wafanyabiashara wa Madini ya Dhahabu ambao wanatuhumiwa  kujishughulisha na utorashaji wa madini wilayani Chunya.

Watuhumiwa hao, wametakiwa kutojishughulisha na shughuli yoyote ya Madini nchini.

Wakati huo huo, Waziri Biteko, ameagiza kuondolewa kwa Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa Madini ya dhahabu anaye husika na usimamizi wa Soko la Madini la Chunya Gagala Poul.

Vile vile, Waziri Biteko amewasimamisha kazi watumishi watatu wa Ofisi ya Madini wa Mkoa wa kimadini wa Chunya baada ya kutuhumiwa kushirikiana na wafanyabiashara kutorosha madini, ambao watumishi hao ni Gabliel Masai, Edward Gavana na George Wandiba.

Pia, Waziri Biteko, ameagiza kusajiliwa kwa Mialo yate inayo chenjua madini ya dhahabu wilayani Chunya ili kujua mwalo gani umezalisha kiasi gani cha dhahabu na dhahabu hiyo imepelekwa kuuzwa soko gani.

“ Bora tubaki na wanunuzi wawili wa madini ya dhahabu ambao ni waanifu kuliko kuwa na mlolongo wa wanunuzi ambao sio waaminifu na wasio fuata kanuni, taratibu na sheria zilizowekwa,” amesema Waziri Biteko.

Waziri Biteko amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila kuwapa zawadi wale wote watakao saidia kupatikana kwa watu wanao torosha madini.

“Niwaombe wachimbaji na wafanyabiashara wote wa madini kutoa ushirikiano kwa Serikali ili kukomesha tatizo la utoroshaji madini, tunataka nidhamu kwenye sekta ya madini ili tulete tija na maendeleo nchini,” amesema Waziri Biteko.   

Pia, Waziri Biteko, amewataka wachimbaji na wafanyabiashara wote wa madini nchini kuhakikisha wanapeleka madini yao sokoni na kuachana na ufanyajibiiashara ya madini nje ya masoko ya madini.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amepongoza Waziri wa Madini kwa kuchaguliwa kuwa mbunge wa Bukombe na kuteuliwa tena kuwa Waziri wa Madini.

Pia, Chalamila amesema Serikali imeshaanza kujenga gereza ili watu  watakao kamatwab wakitorosha madini hawatapekwa mbeya mjini bali watafungwa katika gereza hilo.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: