Thursday, 10 December 2020

WATANZANIA WASHAURIWA KUJENGA TABIA YA KUPENDA BIDHAA ZA NDANI

 


Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Tanzania Growth Trust (TGT), Bi. Anna Domick, Kulia akiangalia bidha iliyotengenezwa na mjasiriamali, Bi.  Maimuna Kinyanile  kushoto  wakati alipotembelea banda la wajasirimali katika maonyesho ya tano ya ya Bidhaa za viwanda vya Tanzania yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwl. JK Nyerere barabara ya Kilwa.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Tanzania Growth Trust (TGT), Bi. Anna Domick, Kulia akifurahia bidha iliyotengenezwa na mjasiriamali, Bi.  Lidya Makanda kushoto  wakati alipotembelea banda la wajasirimali katika maonyesho ya tano ya Bidhaa za viwanda vya Tanzania yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwl. JK Nyerere barabara ya Kilwa.                                    

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam.

KATIKA kuhakikisha viwanda vidogo vidogo vya wajasirimali nchini vinakua, watanzania wametakiwa kujenga tabia ya kutumia bidhaa za ndani ili bidhaa hizo ziweze kupata masoko na kusaidia kukuza uchumi wa taifa.

Rai hiyo ilitolewa jana na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Tanzania Growth Trust (TGT,) Bi. Anna Domick, wakati alipotembelea banda la wajasirimali katika maonyesho ya tano ya bidhaa za viwanda vya Tanzania yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwl. JK Nyerere uliyopo barabara ya Kilwa.

“Wajasiriamali hawa ni zao la TGT ambao waliwezeshwa na Mradi wetu wa Mkubwa. Tunatambua ili uchumi ukuwe ni lazima wawezeshwe na watanzania wapende kutumia bidhaa za ndani,aliongeza kusema, Bi. Domonick.

Alisema taasisi yake inaendesha mradi wa Mkubwa yaani mpango wa kukuza ujasiriamali na biashara kwa wanawake ulioanzisha 2009 ambapo wajasirimali 10,000 wamenufaika.

Alifafanua kwamba taasisi yake imejikita zaidi katika mafunzo ya vitendo, malezi, utengenezaji sabuni, usindikaji wa vyakula, sanaa za mikono na utengenezaji wa batiki, ushonaji wa nguo na ufugaji wa kuku.

Alisema taasisi yake ilifadhili wajasiriamali 15 kushiriki maonyesho hayo ili waweze kuonyesha bidhaa zao na jitihada hizo ni kuunga mkono juhudi za serikali kujenga serikali ya viwanda.

Alisistiza kuwa taasisi za serikali kama TBS, SIDO, GCI, VETA, TANTRADE zinayo nafasi ya kuhakikisha wajasiriamali wadogo, kati na wakulima wadogo wanapiga hatua.

Kauli mbiu ya ya maonyesho yao ina tumia bidhaa za  viwanda vya Tanzania jenga Tanzania.

Naye Mjasiriamali, Bi. Jonecia John alisema yeye ni zao la TGT kupitia mradi wa mkubwa ambapo alimpatiwa ujuzi na vitendea kazi na kwa sasa anatengeneza bidhaa bora.

“Tunataka nchi yetu isonge mbele kupitia viwanda vyetu vidogo vidogo.” Na hapa tunashiriki maonyesho haya ni kutangaza bidhaa zetu na Tanzania ya viwanda, aliongeza kusema, Bi. John.

Alisema bidhaa zao watu wengi waliofila katika maonyesho hayo walishangaa na kuzipenda kuwa watanzania wanauwezo mkubwa wa kuzalisha.

Vilevile Mjasiriamali, Bi. Magreth Msuya  alisema wajasiriamali wanauwezo wa kutengeneza bidhaa bora na zenye ushindani wa ndani na nje ya nchi kikubwa watanzania kupenda bidhaa zao.

Alisema anaiomba serikali kuwakumbuka kwa kuwaandalia maonyesho mara kwa mara ili waweze kuonyesha bidhaa zao.

Alisema taasisi ya mkubwa inayo umuhimu mkubwa  kwa wajasiriamali ambapo inamtoa mtu kutoka katika sifuri hadi katika mafanikio kwa vile inatoa elimu na vitendea kazi hivyo watanzania wajiunge hasa vijana.

No comments:

Post a Comment