Sunday, 13 December 2020

Naibu waziri wa maji Mhandisi Maryprisca mahundi atoa siku mbili kwa Ruwasa

Naibu waziri wa Maji Nchini Meryprisca Mahundi ametoa siku mbili kwa wakala wa Maji Vijijini(Ruwasa) mkoa wa Kilimanjaro kushughulikia changamoto ya Maji na malalamiko juu ya bodi za usimamizi wa Maji Wilaya ya Hai, na kuoewa taarifa ya utekelezaji wake.

Naibu waziri ametoa maagizo hayo leo Disemba 13,2020 wakati wa ziara yake ya Kikazi Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro,  ambapo alipokea taarifa ya hali ya Maji kwa Wilaya hiyo kutoka kwa Mbunge wa Jimbo hilo Saashisha Mafuwe na malalamiko ya usimamizi mbovu wa bodi za maji.

Amesema ni wakati wa watendaji kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kuwajibika ipasavyo kwa wananchi,katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za maji Safi na kwa gharama nafuu.

"Meneja Ruwasa nawapa siku mbili, malalamiko yaliyopo hapa hai ya gharama kubwa ya Maji na mwenendo wa bodi,mshughulikie,naenda Tanga,nikirudi hapa nipewe taarifa,fuatilieni gharama za maji na hata mishahara ya watumishi wa Bodi kwani inalalamikiwa"amesema Mahundi

Awali akizungumza Saashisha Mafuwe,amemueleza Naibu waziri kuwa, hali ya upatikanaji wa Maji katika Wilaya hiyo ni ngumu na kwamba wananchi wengi  wamekuwa wakishindwa kuunganishiwa huduma ya Maji Safi na salama kutokana na gharama kuwa kubwa."Maji ni kilio kikubwa Hai, ili wananchi wafurahi ni wapate maji, pamoja na kwamba upatikanaji wa Maji ni shida,gharama za kuunganishiwa Maji pia ni kubwa, mwananchi anaambiwa atoe zaidi ya Sh 700,000

 Kufungiwa Maji,gharama hii ni kubwa sana,Naibu waziri naomba usaidie katika hili ili wananchi waweze kupata Maji Safi na salama na kwa gharama nafuu"amesema Mafuwe.

Aidha Mafuwe amesema wananchi wamekuwa  wakilazimishwa kununua vifaa vya kuunganishiwa Maji katika maduka ya watumishi wa bodi kwa gharama kubwa na kuiomba serikali kuingikia kati na kutoa uhuru wa wananchi kununua vifaa duka lolote kwa gharama wanayoona ni nafuu kwa kuzingatia viwango ambavyo hutolewa.

Meneja Ruwasa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Weransari Munisi,amesema kigezo ambacho huangalia katika ununuaji wa vifaa vya kuunganisha maji kwa wananchi ni ubora wa vifaa na kuahidi kufuatilia na kulipatia ufumbuzi.Naibu waziri wa Maji Nchini mhandisi Maryprisca Mahundi ametoa siku mbili kwa wakala wa Maji Vijijini(Ruwasa) mkoa wa Kilimanjaro kushughulikia changamoto ya Maji na malalamiko juu ya bodi za usimamizi wa Maji Wilaya ya Hai, na kuoewa taarifa ya utekelezaji wake.

Naibu waziri ametoa maagizo hayo leo Disemba 13,2020 wakati wa ziara yake ya Kikazi Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro,  ambapo alipokea taarifa ya hali ya Maji kwa Wilaya hiyo kutoka kwa Mbunge wa Jimbo hilo Saashisha Mafuwe na malalamiko ya usimamizi mbovu wa bodi za maji.

Amesema ni wakati wa watendaji kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kuwajibika ipasavyo kwa wananchi,katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za maji Safi na kwa gharama nafuu.

"Meneja Ruwasa nawapa siku mbili, malalamiko yaliyopo hapa hai ya gharama kubwa ya Maji na mwenendo wa bodi,mshughulikie,naenda Tanga,nikirudi hapa nipewe taarifa,fuatilieni gharama za maji na hata mishahara ya watumishi wa Bodi kwani inalalamikiwa"amesema Mhandisi Mahundi

Awali akizungumza Saashisha Mafuwe,amemueleza Naibu waziri kuwa, hali ya upatikanaji wa Maji katika Wilaya hiyo ni ngumu na kwamba wananchi wengi  wamekuwa wakishindwa kuunganishiwa huduma ya Maji Safi na salama kutokana na gharama kuwa kubwa."Maji ni kilio kikubwa Hai, ili wananchi wafurahi ni wapate maji, pamoja na kwamba upatikanaji wa Maji ni shida,gharama za kuunganishiwa Maji pia ni kubwa, mwananchi anaambiwa atoe zaidi ya Sh 700,000

 Kufungiwa Maji,gharama hii ni kubwa sana,Naibu waziri naomba usaidie katika hili ili wananchi waweze kupata Maji Safi na salama na kwa gharama nafuu"amesema Mafuwe.

Aidha Mafuwe amesema wananchi wamekuwa  wakilazimishwa kununua vifaa vya kuunganishiwa Maji katika maduka ya watumishi wa bodi kwa gharama kubwa na kuiomba serikali kuingikia kati na kutoa uhuru wa wananchi kununua vifaa duka lolote kwa gharama wanayoona ni nafuu kwa kuzingatia viwango ambavyo hutolewa.

Meneja Ruwasa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Weransari Munisi,amesema kigezo ambacho huangalia katika ununuaji wa vifaa vya kuunganisha maji kwa wananchi ni ubora wa vifaa na kuahidi kufuatilia na kulipatia ufumbuzi.

No comments:

Post a Comment