Sunday, 13 December 2020

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA UTALII AWATAKA WANAHABARI KUFICHUA UJANGILINa Ferdinand Shayo ,Dodoma


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dr.Allan Kijazi amewataka Wanahabari nchini kufichua vitendo vya ujangili wa wanyamapori unaofanywa na baadhi ya watu wasio waaminifu pamoja na kufanya tafiti zitazaosaidia kutokomeza ujangili nchini.


Akifungua Mkutano wa Tanapa Wahariri wa Vyombo vya Habari Jijini Dodoma ,Dr.Kijazi amesema kuwa kuna dalili za  kuibuka kwa aina mpaya ya ujangili wa tembo unaohamasishwa na watu chache wanaohamasisha kuwa  watu maini ya tembo na mafuta yake yanatibu magonjwa ya kansa ya ini na kansa ya kizazi kwa kinamama pamoja na vidonda vya tumbo.


“Aina hii mpya ya ujangili imeibuka  tembo wamekua wakiwekewa mitego na kuuawa huku wakitolewa hivyo viungo ambavyo vinasemekana kidawa ingawa kitaalamu imebainika kuwa maini ya tembo na mafuta sio dawa”


Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Mawasiliano TANAPA ,Pascal Shelutete amesema kuwa wataendelea kuimarisha ulinzi katika hifadhi ili kudhibiti ujangili na kuhakikisha kuwa utali unakua endelevu kwa manufaa ya kizazi kilichopo na kizazi kijacho.


Shelutete amesema kuwa vyombo vya habari vinawajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa wanatangaza vivutio na kusaidia ongezeko la watalii nchini na kufikisha watalii milioni 5 kwa mwaka.


Mwakilishi wa Wahariri wa Vyombo vya habari Mkinga Mkinga ameipongeza Tanapa kwa juhudi wanazozifanya kupiga vita ujangili pamoja na kuhamasisha utalii wa nje na wa ndani.

No comments:

Post a Comment