NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.


Mmiliki wa godaoni la wauzaji vyuma chakavu na wazazi wa watoto watatu waliokuwa wakikabiliwa natuhuma kuiba viti 108 vya shule ya sekondari Sinoni na kuuza kama vyuma chakavu wamelipa kiasi cha shilingi  milion tano na  laki nne kwaajili ya kutengeneza viti vipya meza.



Akizungumza Mmiliki wa godaoni hilo Yuda kamando amesema kuwa wanakiri tatizo hilo kutokea hivyo wanaomba radhi serikali na wamelipa gharama ya shilingi milion 5 na laki nne kwaajili ya kufidia viti hivyo 


Akisema kuwa atahakikisha  wafanyakazi wake hawanunui Mali za serikali pamoja na za wizi kwani tukio hilo limemfanya kupata uzoefu wa kulinda na kusimamia   vizuri wafanyakazi wake.


Mmoja kati ya wazazi wa wanafunzi hao Saruni Laizer ameleza   namna watakavyo hakikisha watoto hao wana achana na tabia ya wizi ili waendelee na masomo kwa ufanisi kwani tatizo hilo linaweza kuwapelekea kujiingiza katika ujambazi.


" Tutatuwa na ukaribu  na watoto wetu pamoja na walimu ili kuhakikisha wanafanya vizuri katika masomo yao  ili kufikia ndoto zao tutawafuatili kwanzi wanapokwenda shule,wakiwa darasani na wanapotoka," alisema Laizer


Kwa upande wake mkuu wa wilaya Kenani Kihongosi alisema kuwa anawashukuru kwa kuchangia fedha hizo kwani wameonesha ushirikiano na serikali katika changamoto hiyo hivyo fedha hizo  zitaenda kutengeneza viti vingine 108.


Aidha amewataka wazazi  kuwajibika vyema katika malezi ya watoto wao kwani wazazi wanachangia kuharibu tabia za watoto hao pamoja na wafanyabiashara kuacha kununu bidhaa za vyuma kwa watoto wadogo.


" Wafanyabiashara  wa vyuma chakavu waache kununua  mali za serikali kwani tutawachukulia sheria kali hna jambo hilo linatokana na kukosekana kwa uzalendo wa nchi yao"


Hata hivyo amewataka maafisa elimu,bodi za shule na viongo wengine  kuhakiki mali za shule ikiwemo viti kwaajili ya kujirizisha kila baada ya mwezi mmoja ili kuondoa sakata hilo la upotevu wa ka  viti.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: