Pichani ni sehemu ya mahindi yaliopelekea Alex Minja kuuawa


Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro limetakiwa kufanya uchunguzi wa kina Mara baada ya kijana Alexi Alfred Minja mwenye umri wa mika 29 mkazi wa Marangu Magharibi kijiji cha malambu Mkoani Kilimanjaro kuuawa kikatili kwa madai ya kuiba Mahindi kwenye shamba la Jirani yake 


Akizungumza msemaji wa familia ya Minja kuhusu kuawa kwa mwanae Bwana Agustino Thadey Minja anasema kwamba Marehemu alipigwa na wananchi kwa kutumia magogo makubwa kumpiga kichwani na kumsababishia kuvuja damu nyingi eneo la kichwa na kupoteza maisha 

Minja amelezea kwamba mwanae huyu alikuwa hana tabia ya wizi ila kinacho onekana ni chuki na wivu wa maendeleo ndio kilicho sababisha kijana wake kupoteza maisha na sio kweli kwamba ameiba mahindi kwani kijijini hapo Marangu Magharibi wanamiliki shamba kubwa lenye mahindi 

Ndugu zangu waandishi kiukweli tumefika hapa nyumbani nakukuta ndugu yetu tayari ameisha uawa na watu wasiojulikana hivyo tunaliomba jeshi la Polisi kufanya uchunguzi kuweza kubaini ninani walio husika na mauaji ya mwanae kwani mpaka sasa ni siku ya nne mwili uko hospital na hatujui ni lini tutamzika maana mpaka sasa mwili haujafanyiwa uchunguzi wowote alisema baba mkubwa wa marehemu Agustino Minja 

Amesema wanacho omba kwa jeshi la Polisi ni kukamatwa kwa watuhumiwa kwani wanatamba mtaani kufanya mauaji na hakuna wa kuweza kuwafanya lolote hivyo sheria ichukue mkondo wake wabainike wahalifu na kufikishwa katika mikono ya sheria.

Naye Shangazi yake marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Magret Thadey Minja amesema alipigiwa simu akiwa Mkoani morogoro na kupewa taarifa kwamba Shangazi yake ameuawa kikatili kwa kupigwa na watu Wa sio julikana kwa madai ya kuiba mahindi 

Shangazi Magret alieleza kwamba hata kama kulikuwepo na wizi kusingetakiwa kujichukilia sheria mkononi kulipaswa marehemu apelekwe Polisi pamoja na kidhibiti cha wizi wa mahindi na kufunguliwa mashtaka na sio kupigwa kwa muda wa Masaa saba bila kupumzishwa hadi kufariki dunia 

Amesema kwamba Watuhumiwa walifanya tukio hilo kinyama kwani hakuna mtu 

yoyote aliyeshuhudia mauaji hayo hivyo inawezekana ameawa na watu ambao pia ni majambazi na sio watu  wasiofahamika 

Baadhi ya majirani walisema walisikia kelele zikipigwa nje kwa muda mrefu na kujua kwamba ni ugomvi wa vijana wa kawaida tu lakini baadae walisikia zimezidi na kutoka nje na kukuta ni Alexi amepigwa na walipo muliza alijibu kuna watu wamenivamia wamenipiga na kuondoka baada ya muda alifariki dunia 

Kaimu Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro Ronald Makona amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na mpaka Sasa baadhi ya watu wasiopungua watatu wanashikiliwa kwa mahojiano na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani huku akiitaka familia hiyo kuwa wavumilivu katika kipindi Cha uchunguzi wa tukio hilo.

Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: