Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Joseph Nyamhanga ,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Ofisini kwake jijini Dodoma akitangaza ajira zipatazo 13,000  za walimu kwa  shule za msingi na Sekondari.Kuona majina,bofya hapa MAJINA YA WALIMU_compressed.pdf

Baadhi ya watumishi wa Elimu kutoka Ofisi hiyo wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Joseph Nyamhanga (hayupo pichani) wakati akitangaza ajira zipatazo 13,000  za walimu kwa  shule za msingi na Sekondari jijini Dodoma.

Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Joseph Nyamhanga (hayupo pichani) wakati akitangaza ajira zipatazo 13,000  za walimu kwa  shule za msingi na Sekondari jijini Dodoma.

…………………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Joseph Nyamhanga ,ametangaza ajira za walimu wa shule za msingi na Sekondari zipatazo 13,000 huku akiwataka wote walioweza kupata ajira hizo kuripoti ndani ya muda uliopangwa.

Akitangaza mbele ya waandishi wa habari jijini Dodoma Mhandisi Nyamhanga amesema kuwa walimu hao wanapaswa kuripoti ndani ya siku 14 kuanzia Desemba Mosi hadi 14 na wale ambao watashindwa kuripoti ndani ya muda huo nafasi zao zitachukuliwa na walimu wengine.

Mhandisi Nyamhanga amewataka wote walioteuliwa kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi ambavyo ni shule za msingi na sekondari na siyo kuripoti katika ofisi za halmashauri huku akitoa onyo kwa wale watakaochukua posho za kujikimu kwa siku saba watakazoenda kuripoti afu wasitokee kuwa watachukuliwa hatua za kisheria.

Aidha Nyamhanga amesema kuwa  kwa mara ya kwanza Serikali imetoa ajira kwa kundi la walimu wenye shahada ya ualimu kwa ajili ya shule za msingi ambapo walimu hao ni wale wa masomo ya sanaaa ambao wapo 1,100 na hiyo ni kwa sababu shule za sekondari hazina uhitaji mkubwa wa walimu wa mchepuo huo.

Mhandisi Nyamhanga amesema asilimia 60 ya walimu wote walioajiriwa wamepelekwa shule za msingi hasa za vijijini kwenye uhitaji mkubwa wa walimu.

” Kuanzia leo jioni wote waliofanya maombi wapite kwenye tovuti yetu watakutana na majina yao, kwenye shule za msingi tumechukua walimu kwenye makundi manne ambapo kundi la kwanza ni wale wenye daraja la 3A astashahada, kundi la pili daraja la 3B astashahada, kundi la tatu ni daraja la 3C shahada na kundi la nne ni daraja la 2B na C.

Kwa Sekondari  walimu ni asilimi 40 ambapo wapo kwenye makundi saba ambao ni daraja la 3B stashahada kundi la pili 3C shahada, kundi la tatu ni daraja la 3C shahada, kundi la nne ni daraja la 3C shahada wakati kundi la tano ni daraja la tank 3B na daraja la 3C,” Amesema Mhandisi Nyamhanga.

Amesema pia wamezingatia shule zenye mahitaji maalum ambapo walimu 481 wameajiriwa kwa ajili ya shule hizo na kuongeza kuwa suala la umri wa ajira za serikali limezingatiwa na walimu waliopata ajira ni wale walioajiriwa ni wale waliomaliza Chuo mwaka 2014 – 2019.

Kuona majina,bofya hapa MAJINA YA WALIMU_compressed.pdf

 

Share To:

msumbanews

Post A Comment: