Na,Jusline Marco;Arusha


Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Richard Kwitega amezindua dawati la mfano la ulinzi wa mtoto shuleni litakaloshughulika na masuala ya ulinzi na usalama wa haki za mtoto pindi awapo shuleni.

Akizindua dawati hilo katika Siku ya Kimataifa ya Mtoto iliyofanyika jijini Arusha,Kwitega amesema kuwa zaidi ya watoto milioni 20 nchini wanakadiriwa kuwa na  miaka chini ya 18 sawa na asilimia 50 ambao kati yao hukabiliwa na vitendo vya ukatili wa kinjisia na kingono amnapo amesema watoto wana sehemu kubwa ya jamii katika nchi ya Tanzania kwani maendeleo ya taifa lolote ulimwenguni hutokana na namna walivyowandaa watoto hao.

Aidha ameeleza kuwa siku hiyo kimataifa ya mtoto inatoa wajibu kwa kila mdau wa mtoto kutetea na kulinda haki za mtoto sambamba na kutafsiri kwa vitendo maelekezo ya mikataba ya kimataifa yenye lengo la kuwezesha ulimwengu bora kwa watoto ambapo amesema kauli mbiu ya mwaka huu inahimiza jamii umuhimu wa kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya kikatili.

Vilevile amesema kuwa mnamo mwaka 1959 Baraza kuu la umoja wa mataifa lilipitisha azimio la haki ya mtoto ambapo mwaka 1989 mwezi Novemba Baraka kuu la usalama la umoja wa mataifa lilipitisha kwapamoja mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto kipitia azimio namba 198 la mwaka 1979 ambapo kuanzia mwaka 1990 siku ya kimataifa ya mtoto ikaanza kuazimishwa na mataifa mbalimbali duniani.

"Kwa mujibu wa azimio la haki za watoto la mwaka 1989 la umoja wa mataifa ambalo liliridhiwa na serikali ya Tanzania mwaka 1991 azimio hilo limetoa misingi 4 muhimu ya haki za watoto ikiwemo haki ya kuishi na kulindwa,haki ya mahitaji muhimu ya mtoto,haki ya kutobaguliwa pamoja na haki ya kushirikishwa."Alisema Kwitega

Kwa upande wake mratibu wa haki za watoto na vijana Taifa kupitia Shirika la SOS Tanzania,Mpeli Ally Kalonge amesema kuwa maadhimisho hayo yanatoa fursa kwa nchi wanachama kutetea haki za mtoto ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanaweka misingi mizuri ya usalama na ulinzi wa mtoto ili aweze kipata haki zake za msingi.

Mpeli ameongeza kuwa kwa kushirikiana na wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto wamekutanisha watoto zaidi ya 250 kutoka katika mashirika mbalimbali na kutoa nafasi kwao kujadili na kuweza kuona hali ya usalama na ulinzi wao ikoje kuanzia ngazi ya familia,halmashauri,wilaya hadi mkoa kwa kuangalia upatikanaji wa haki zao kuu tano.

Akizungumza kwa niaba ya watoto wenzake katika maadhimisho hayo,Mtoto Brais Wilson amesema kuwa mbali na changamoto zinazowakumba watoto pindi wawapo shuleni,njiani,nyumbani na katika jamii ambazo ni ubaguzi wa wanafunzi,udhalilishaji wa wanafunzi,ubakaji,kushawishiwa kufanya mambo yaliyoko nje ya uwezo wa mwanafunzi au mtoto,ukatili wa kijinsia,kutopewa haki aa msingi,ajira za utotoni,ndoa na mimba za utotoni zinazotoka na mtoto wa kike kulazimishwa kuolewa akiwa na umri mdogo pamoja na kulawitiwa.

Pamoja na uwepo wa changamoto hizo,Brais ameeleza mikakati ambayo inapaswa chukuliwa ili kuweza kutokomeza changamoto hizo ambazo ni utoaji wa semina ya kuelimisha jamii kuhusu wanafunzi na watoto kupewa ulinzi sambamba na kushawishiwa kuendelea kusoma ili maisha yao ya baadae yaweze kuwa mazuri,kutowatenga watoto wenye ulemavu, ambapo amewaomba wadau mbalimbali kuwajali watoto wa mitaani kwa kuwapa elimu madhubuti itakayowaondoa katika hali hiyo.
Share To:

Post A Comment: