Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa kushoto akimkabidhi msaada wa taulo za kike Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga(RAS) Judica Omari katika kwa ajili ya wasichana kwenye shule ya Sekondari Old Tanga zenye thamani ya Milioni 5,kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Old Tanga Kasimu Ndumbo  wa kwanza kulia ni Afisa Elimu Mkoa wa Tanga Mayansa Hashimu na wa kwanza kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) Faidha Salim
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa kushoto akimkabidhi msaada wa taulo za kike Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga(RAS) Judica Omari katika kwa ajili ya wasichana kwenye shule ya Sekondari Old Tanga zenye thamani ya Milioni 5,kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Old Tanga Kasimu Ndumbo  wa kwanza kushoto  ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) Faidha Salim
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa akizungumza wakati wa halfa hiyo ya makabidhiano
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari akizungumza wakati wa halfa hiyo
AFISA Elimu Mkoa wa Tanga Mayansa Hashimu akizungumza wakati wa halfa hiyo

Meza kuu wakiwa wamesimama wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kupokea msaada huo

Sehemu ya walimu na wanafunzi wa shule ya Sekondari Old Tanga wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye halfa hiyo
Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Old Tanga akitumbuiza kwenye halfa ya makabidhiano hayo
 Wanafunzi wa shule ya Sekondari Old Tanga wakiiimba wimbo wa Taifa kabla ya kupokea msaada huo

BENKI ya CRDB imetoa msaada wa taulo za kike zenye thamani ya sh.milioni 5 katika shule ya Sekondari Old Tanga ya Jijini Tanga ili kuwasaidia watoto wa kike kusoma kwenye mazingira salama hali itakayowasaidia kuongeza bidii kwenye masomo yao.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano hayo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari, Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa alisema kwamba wametoa msaada huo kupitia kampeni maalumu ya Hedhi Salama kwa elimu bora.

Alisema kwamba Benki ya CRDB inachukua kwa uzito sana suala la uwezeshwaji mtoto wa kike,mwanamke hatua ambayo imepelekea benki yao kutunga na kutekeleza sera na mikakati inayolenga kuhamaisha usawa wa kijinsia na kutengeneza mazingira rafiki kwa mwanamke.

Meneja huyo alisema kwamba ndani ya benki yao wamefanya hivyo wakiamini kuwa ukimuewezesha mwananke umeiwezesha jamii na hivyo ndio moja ya siri kubwa ya mafanikio kwenye benki hiyo.

Alisema benki hiyo waliamua kuanzisha mpango huo lakini kwa bahati kubwa shule ya Sekondari Old Tanga wakawa ni miongoni mwa shule ambazo wanaanza nazo.

“Pamoja na jitihada zinazofanywa na wadau mbalimbali ikiwemo serikali bado mahudhuria ya watoto wa kike mashuleni hayaridhishi na hivyo kupelekea kutokufanya vizuri katika masomo yao “Alisema

Alisema changamoto hiyo kwa kiasi kubwa imechangia watoto wengi wa kike wakati wanapoingia kwenye kipindi chao cha hedhi kutokuwa na uwezo wa kuwa na taulo bora za kike inawalazimu kukaa nyumbani na kushindwa kwenda shule na kukaa nyumbani mpaka watakapomaliza .

Meneja huyo alisema lakini au kuvaa vitambaa ambavyo sio salama kwa afya zao ambapo alieleza kwamba utafiti uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya Magonjwa ya Binadamu NIMR unaonyesha kuwa katika wilaya 14 za Tanzania Bara ulibaini kuwa asilimia 15 ya wanafunzi wa kike wanashindwa kuhudhuria shule katika siku zao za hedhi.

Alisema katika ya hizo asilimia 42 inachangiwa na ukosefu wa vifaa vya hedhi na 34 asilimia hofu ya kujichafua kwa sababu hana kitu sahihi cha kujistiri huku asilimia 26 inatokana na miundombinu isiyokuwa rafiki wakati akiwa kwenye kipindi cha siku zake.

“Kutokana na changamoto hiyo benki ya CRDB tuliamua kuanzisha kampeni maalumu ijulikanayo Hedhi Salama kwa elimu bora inayolenga kutatua changamoto wanazopata watoto wa kike kwa kutoa msaada wa taulo za kike kwenye shule mbalimbali nchi nzima”Alisema

Aliongeza kwamba wao kama benki wanaamini upatikanaji wa taulo za kike ni muhimu kwa mahudhurio ya mtoto wa kike shuleni na kupata haki yake ya msingi wa elimu sawa na mtoto wa kiume

Awali akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari aliwashukuru Benki ya CRDB kutoa msaada huo ambao utasaidia katika kuboresha masomo yao.

“Kwa kweli niwashukuru sana na kuwapongeza uongozi wa Benki ya RCD kwa kutambua umuhimu wa huduma hii kwa mtoto wa kike kwenye mkoa wa Tanga nimefurahihwa sana kwa kujali na kutoa mahitaji haya ambayo ni muhimu kwa vijana wetu wa kike”Alisema Ras Judica.

Aidha alisema kwamba serikali ya awamu ya tano nchini ya Rais Dkt John Magufuli inatoa kipaumbele kwenye kuboresha elimu na shule nyingi zimepewa kipaumbele cha hali ya juu.

Alisema katikampango wa elimu ya bila malipo imeongeza zaidi idadi ya wanafunzi kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha kwanza na ufadhili huo ambao umepatikana ni mkubwa kutokana kwa serikali ya awamu ya tano huku akieleza kwamba kwa mkoa wa Tanga umeendelea kupokea msaada huo.

Katibu Tawala huyo alisema kila mwezi kwa mkoa wa Tanga wanapokea kiasi cha sh.Bilioni 1 kwa ajili ya kuendesha mpango wa elimu bure katika shule na mpango huo unasaidia katika kutoa posho mbalimbali kwa ajili ya uwezeshwaji wa wanafunzi, wakuu wa shule wanawezeshwa

Alitaja pia uwezeshwaji wa walimu wakuu pamoja na maafisa elimu kata ambao ni viongozi muhimu katika kuhakikisha elimu bora inapatikana mkoani

“Katika ngazi ya shule fedha hizo pia zinatumika kwenye masuala ya kujenga taaluma, kufanya ukarabati, utawala, kununua vifaa, usimamizi mitihani katika hiyo fedha pa asilimia 10 inatumika kwenye kununua mahitaji mbalimbali kwa ajili ya kumuwezesha mtoto wa kike kuweza kufanya ufaulu mzurina kuweza kukaa shuleni kwa utulivu”Alisema




Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: