Na John Walter-Babati

Watu wenye ulemavu Wilayani Babati Mkoani Manyarawamepatiwa elimu ya mpiga kura itakayowawezesha kushiriki vyema katika zoezi la kupiga kura Octoba 28 mwaka huu na pia kutambua vipaumbele walivyopewa na tume ya uchaguzi pindi wanapofika katika vituo vya kupigia kura.

Akizungumza na Makundi ya watu wenye ulemavu Wilayani Babati mkoani ManyaraMkurugenzi wa asasi ya Kiraia yaa COSITA,Patrice Gwasma   alisema kuwa wameamua kutoa elimu hiyo ili waweze kutumia haki yao ya kikatiba ya kuchagua kiongozi wanayemtaka atakayepigania maslahi yao.

Gwasma alisema kuwa kundi hilo muhimu linahitaji kupata elimu ya  mpiga kura na kuhamasishwa umuhimu wa kushiriki katika zoezi la uchaguzi .

“Tume imetoa kipaumbele cha kuwahudumiamapema walemavu aina zote, hii inaonyesha jinsi gani makundi haya yanapata fursa za kupiga kura bila usumbufu huku wakizingatia sharia za uchaguzi”  Alisema Mkurugenzi.

Mwenyekiti  wa Shirikisho la Vyama vya watu  wenyeulemavu Mkoa wa Manyara (SHIVYAWATA) JosephMasasi amepongeza asasi hiyo ya kiraia  kwa kutimiza wajibu wa kutoa elimu ya Mpiga kurahususan kwa walemavu kundi ambalo limekua likisahaulika mara kwa mara .

Kwa upande wao walemavu  waliopata elimu hiyo,wameiomba serikali kuwepo watu wenye uwezo wakuwaongoza wenye ulemavu wa macho kuwezakuwachagua watu wanaowahitaji.

Aidha wameomba kutengewa mazingira rafikiyatakayowawezesha kupiga kura bila kikwazo.

Aidha Wameishukuru Taasisi ya COSITA kwakuwawezesha kupata mafunzo hayo kwa kuwa elimu hiyo itawasaidiakutumia haki yao ya kikatibakuchagua viongozi bora na kuyaomba mashirikamengine kufika vijijini na wilaya za pembezoni ili kuwafikia walemavu wengi zaidi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: