Wawakilishi wa Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayoendelea katika Uwanja wa Kituo cha Uwekezaji Bombambili Mjini Geita, wamefanya ziara katika mgodi wa mfano wa Lwamgasa uliopo Wilayani Geita Mkoani Geita kwa ajili ya kujifunza namna mgodi huo unavyoendesha shughuli zake kwa lengo la kuwasaidia wachimbaji wadogo.

Akizungumza na wawakilishi hao msimamizi wa mgodi huo, Victor Olal amesema kuwa lengo la mgodi ni kutoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini sambamba na kutoa huduma ya uchenjuaji wa madini kwa wachimbaji wanaofika mgodini hapo kwa ajili ya kupata huduma hiyo.

Zifuatazo ni picha za matukio mbalimbali.





Share To:

msumbanews

Post A Comment: