Monday, 28 September 2020

WAFUGAJI WAAHIDI USHINDI KWA RAIS MAGUFULI


NA MWANDISHI WETU ARUSHA

CHAMA cha Wafugaji Tanzania (CCWT) kimewaomba wananchi wa wilaya ya Ngorongoro iliyopo mkoani Arusha kumchagua mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk, John Magufuli ili awasaidie kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo baadhi ya wananchi kutakiwa kuhama kwenye maeneo yao ya asili.


Aidha wananchi hao wamesema kwamba wilaya ya Ngorongoro itaongoza kitaifa kwa kumpa kura za "NDIYO" mgombea urais wa CCM Dk, Magufuli ambaye pia ni Rais wa Tanzania.


Ombi hilo limetolewa mwishoni mwa wiki na mwenyekiti wa CCWT Taifa Jeremia Wambura wakati wa ziara yake ya  kikazi katika  tarafa ya Ngorongoro  iliyopo  ndani ya Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ambapo wanachi  hao ambao ni wafugaji walimalalamikia juu  ya kero mbalimbali zinazotokana na mamlaka hiyo.


"Wafugaji wenzangu nimesikia kero zenu nyingi zinazotokana na NCAA ikiwemo baadhi yenu kutakiwa kuhama kwenye maeneo yenu ya asili mliyokuwa mnaishi,ukosefu wa chumvi kwa ajili ya mifugo pamoja na chakula kwa kuwa hamaruhusiwi kulima.Lakini mwarobaini wa kero hizi ni Dk, Magufuli hivyo nawaomba sana Oktoba 28  mwaka huu tumchague na nitahakikisha baada ya ushindi kundi la kwanza atakalokutana nalo ni wafugaji".

Kuhusu kero ya baadhi ya wananchi kujeruhiwa na wanyama bila kulipwa fidia Wambura aliitaka NCAA kulipa fidia mara moja kwa wafugaji hao kwa kuwa wanaishi na wanyama na ikiwa ni pamoja na kuwalinda dhidi ya watu wenye nia ovu.


"Sifa kubwa ya NCAA ambayo haipatikani mahali popote dunia zaidi ya hapa Ngorongoro ni wanyama ,mifugo na binadamu kuishi pamoja.Hivyo hakikisheni mnalipa fidia kwa wnachi wanaojeruhiwa na wanyama kwa sababu wao ninsehemu ya uhifadhi lakini pia kivutuo cha utalii katika eneo hili".


Awali akizungumza kwa niaba ya wanachi hao mwenyekiti wa baraza la  wafugaji tarafa ya Ngorongoro Edward Maura alisema  NCAA imekaidi agizo la waziri mkuu Kassim Mjliwa alilolitoa Disemba mwaka 206 wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani humo ambapo mifugo haitashuka tena Kreta kunywa maji na chumvi na badala yake NCAA inunue chumvi kwa ajili ya mifugo pamoja na  kujenga mbauti za mifugo kunywea maji.


Alisema ukosefu huo wa chumvi umesabisha mifugo kukojoa damu na kwamba  zaidi ya  70,000 imekufa  huku mingine ikiwa inashindwa kubeba mimba .

 Alisema uongozi wa NCAA umeaniasha maeneo na kuyapa jina la "No go Zone" bila kushirikisha wananchi wa  maneo hayo na kuwataka kuondoka maeneo hayo ambayo yana malisho ya mifugo pamoja na huduma nyingine muhimu.

"Uongozi wa NCAA umekuwa ukikiuka taratibu za sisi wanachi kuishi ndani ya eneo hili kwa sababu hakuna ushirikishwaji wa jambo lolote licga ya sisi kuwa wadau wakubwa katika eneo hili badala yake tunapewa notsi za kututaka kuondoka kwenye  maeneo yetu ya asili ambayo NCAA imeyapa jina la "No Go Zone."


Akizungumzia ushindi wa Mgombea urais wa CCM Dk, Magufuli alisema wamejipanga kukamilifu kuhakikisha kwamba wilaya ya Ngorongoro inaongoza kwa kura za Rais kwa nchi nzima.


"Tunaomba kukuhakikishia kwamba licha ya changamoto zetu wilaya ya  Ngorongoro tutaongoza kitaifa kwa kumpigia kura Magufuli na ushindi wake ni asilimia mia moja na kwamba wagombea urais watapata kura sifuri.


Tate Olelepayan alidai kuwa wananchi wanateseka kwa kukosa lishe bora kwa kuwa hawaruhusiwi kilimo cha kujikimu na kwamba wanapewa mahindi kilo 25 kwa kaya moja ambayo hayakidhi mahitaji familia .

"Tunateseka kwa njaa na kukosa mlo bora.NCAA inatupa kilo 25 za mahidi kwa kaya moja kwa mwezi mmoja chakula ambacho hakikidhi mahitaji.Kama hawawezi kutuletea mahindi, maharage na mafuta ni bora wakaacha kuliko kuidanganya serikali kuwa wanatupa chakula cha kujikimu".

Akijibu malalamiko hayo Naibu Kamishna wa uhifadhi  NCAA Ephrahim Mwangomo alisema hakuna  mtu yeyote wa Tarafa ya Ngorongoro atakayehamishwa na hakuna mtu wa kumtushia mwananchi chini ya uongozi wa Rais John Magufuli.

"Katika uongozi wa JPM hakuna mtu atakaye hamamishwa Tarafa ya Ngorongoro kwa kuwa Rais John Magufuli hataki wananchi wake waonewe kwa namna yeyote na sisi kama NCAA tutasimamia kikamilifu".

Kuhusu wananchi kukosa chakula Meneja Maendeleo ya  jamii wa NCAA Fedes Mdala alikiri kwamba mamlaka hiyo inatoa mahindi pekee kwa wananchi hao na kwamba mwaka 2022 itaacha kabisa kutoa mahindi  kwa wananchi hao.


"Ni kweli  NCAA tunawapa mahindi tuu na ni vigumu kutoa chakula cha kutosha kwa wananchi wote na mwaka 2022 tutawatafutia mashamba nje ya eneo hili ili wakalime kwa ajili ya kujipatia chakula cha uhakika".

Akijibu hoja ya kukaidi agizo la Waziri Mkuu Mdala alikiri ni kweli baadhi ya vijiji havijapata chumvi na kwamba tangu agizo hilo litolewe ni vijiji vitatu pekee vya Erikapusi,Nayobi na Olorobi na kuahidi kuwa mwezi Oktoba mwaka huu mifugo itapata chumvi kwa kuwa wametenga milioni 40 kwa ajili ya chumvi licha ya bajeti hiyo kuathiriwa na COVID19 iliyoshusha mapato yao kutokana na kutokuwa na watalii.


 Akijibu hoja ya wananchi kutolipwa fidia aliwaomba wananchi waliojeruhiwa kuwasilisha ofisini kwake malalamiko hayo ili ayafanyie kazi.

No comments:

Post a comment